Ticker

6/recent/ticker-posts

RC TABORA AAGIZA TARI –TUMBI KUZALISHA MICHE YA MITI ASILI YA MATUNDA PORI NA DAWA

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani(kulia)  akiangalia leo mmoja ya mahindi ambayo yamezalishwa na Watafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI) kwa ajili ya mbegu bora. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi Dkt . Emmanuel Mrema Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani(kushoto)  akiangalia leo kili mbili za mbegu bora ya mahindi yaliyozalishwa na Watafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI) kwa ajili ya mbegu bora. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi Dkt . Emmanuel Mrema Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi Dkt . Emmanuel Mrema(kushoto) akimwonyesha leo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani(kulia)  miche ya michikichi ambayo imezalishwa na Watafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI) kwa ajili ya mbegu bora.
 

Na  Tiganya Vincent

RS-Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani  amewaagiza Watafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI) kuhakikisha wanaendelea na uzalishaji wa miche miti asili ya matunda na dawa kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi.

Amesema nchi nyingi matunda pori yana thamani kubwa sana kwa kuwa yatumika kutengenezea vitu mbalimbali ikiwemo mvinyo.

Balozi Dkt. Batilda alitoa agizo hilo leo wakati akipokuwa na ziara ya kikazi katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI)

Amesema Watafiti hao wakasaidia katika kuhakikisha kasi ya upandaji wa miti ya dawa za asili na matunda pori inaongezeka katika jamii kwa ajili ya kuhakikisha kuwa haipotei.

Balozi Dkt. Batilda amesema kwenye matunda pori kuna vitu vingi ikiwemo lishe ambayo ni muhimu kwa ajili ya afya za wananchi.

Amesema kwa TARI wamefanya utafiti na kuonyesha matunda pori yanawezekana kupandwa katika maeneo ya Mkoa wa Tabora ni vena elimu hiyo pia ipelekwe kwa wananchi nao pia waweze kushiriki katika upandaji.


Post a Comment

0 Comments