Ticker

6/recent/ticker-posts

DC MURO KUTENGUA KITENDAWILI CHA MGOGORO WA HIFADHI YA MSITU WA MINYUGHE WENYE HEKTA 400,000

Changamoto kubwa inayonikabili kwa sasa ni mgogoro kati ya wananchi wa tarafa ya sepuka yenye kata 6 zenye changamoto na hifadhi ya msitu wa minyughe ambao mchakato wa kuuihifadhi ulianza mwaka 1992 ambapo Wizara ya Maliasili ilituma wataalamu kuupima na eneo lililopimwa lilikuwa na ukubwa wa Hekta 400,000


Katika kukabiliana na changamoto hii nimeona ni busara kwanza kujiridhisha na taarifa nilizopewa Kuhusu mgogoro huu na katika kujiridhisha nimeona nianze na ziara nikiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mzee Ally Mwanga pamoja na Viongozi wa TFS wenye dhamana na misitu pamoja na Viongozi wa Wananchi, Madiwani na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji

Hii ni ziara ya kutembelea, kukagua,maeneo yote yenye changamoto


Mara baada ya ziara tutakaa pamoja kwenye kikao cha pamoja cha kutafuta muafaka, na kubwa ni kutoa nafasi ya kuwa na mjadala wa pamoja baina yetu Viongozi wa Serikali, wawakilishi wa Wananchi pamoja na wenzetu wa TFS na kisha tutatoka na muafaka wa pamoja ambao utamaliza changamoto hii kabisa 


Leo nimeanza na kata ya Mwaru kijiji cha mpugizi kitongoji cha mkondogwa jimbo la Singida Magharibi, kutoka Makao Makuu ya Wilaya ya Ikungi mpaka huku ni umbali wa Km 220 kazi inaendelea 


Imetolewa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya IkungiPost a Comment

0 Comments