MKURUGENZI wa Jiji la Tanga Sipora Liana akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji hilo leo |
Madiwani wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye kikao hicho
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa kikao hicho
DIWANI wa Kata ya Msambweni (CCM) Godias Kimath kushoto akifuatilia kwa umakini kikao hicho
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Spora Liana wakati wa kikao cha robo ya nne cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji hilo ambapo amewataka watendaji hao kujipima na kujitathimini kama wanatosha kwenye nafasi zao.
Alisema
kwamba wao watendaji wapo kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi hivyo
wahakikishe wanafanya tufanye vitu vya kuwasaidia ili kuweza kukuza
uchumi wao ambao utakuwa chachu ya kuweza kujikwamua kimaendeleo
"Lakini tusisubiri mpaka wananchi waone na waseme kwamba kweli Halmashauri yao ipo kwa hiyo watendaji na wakuu wa idara kaeni mkao wa kujipima,je tunatoshaa? waananchi ndio wanaotupima kama tunatosha au hatutoshi na Mh.Dc yupo hapa kusimamia na kuhakikisha kwamba kila kitu kinatekelezwa"Alisema Spora
Mkurugenzi huyo aliongeza kwamba watendaji wapo kuwawakilisha wananchi hivyo ni muhimu kuona namna ya kushirikiana nao ikiwemo kuwaeleza fursa zilizopo katika jiji la Tanga ambazo zitawaongezea kipato.
Hata hivyo alisema lazima waangalia ni namna gani wananchi watatoka hapo walipo kwa kujiandaa na fursa mbalimbali ikiwemo mradi mkubwa wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda Hadi Tanga.
Alisema ni muhimu wajue ni vitu gani vitaambatana na bomba la mafuta vitakavyowasaidia kwenye maeneo yapi watayatumia kuwasaidia wananchi kwa sababu wapo hapo kwa ajili ya wananchi .
Halmashauri ya jiji la Tanga imedhamiria kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuibua vyanzo vipya vya mapato.
0 Comments