Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro ameitaka jamii kujiepusha
na kuacha vitendo vya udhalilishaji na biashara ya dawa za kulevya kwani vyombo
vya dola vitatumia sheria zilizopo kuwashughulikia wanaojihusisha na vitendo
hivyo.
IGP Sirro amesema hayo leo wakati akifunga mafunzo ya uongozi mdogo wa Cheo
cha Sajenti wa Polisi yaliyofanyika kwa muda wa miezi miwili katika Chuo cha
Polisi Zanzibar ambapo jumla ya wahitimu 1297 walihitimu mafunzo hayo na
kupandishwa vyeo.
0 Comments