Ticker

6/recent/ticker-posts

MATEMBEZI KUOMBOLEZA KIFO CHA MJUKUU WA MTUME MUHAMMAD




Jumuiya ya Khoja Shia Ithanasheri wafanya matembezi ya kuomboleza kifo cha mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Imam Hussain (as) aliyeuawa Karbala, Iraq , siku ya Ashura.

Ashura ni siku ya kumi ya mwezi mtukufuwa Muharram. Zaidi ya Miaka 1300 iliopita, Katika siku hii ya Ashura mjukuu wa Mtume yaani Imam Hussain (as) aliuawa katika tambarare za mji wa Karbala, Iraq.


Alisimama kidete dhidi ya mtawala dhalimu wa wakati ule, Yazid bin Muawiya, akatoa fundisho la kukataa kumpigia magoti mdhalimu huyo, Ndipo akajitolea maisha yake, akauawa ili kunusuru ubinaadamu na utu.
Siku hii huadhimishwa kila mwaka, ili kuingiza thamani ya mafundisho hayo, ndani ya nafsi zetu. Imam Hussain (a.s) alisimamia; Kuamrisha mema na kukataza mabaya. “Amr bil Marouf na Nahyanil Munkar”.




Utauliza kwanini kuna matembezi haya leo katika ardhi ya Tanzania?
Ni Kwa sababu ya ujumbe wa amani aliyokuwa amebeba Imam Hussain (as), Naye anaeleza, Mimi sikua sikwauovu au tabia mbaya wala kutafuta umaarufu bali nilinyanyuka kutafuta kusawazisha mwenendo takatifu la babu yangu, ambaye ni mjumbe wa Allah (swt).


Imam Hussain(as), ni moja katika masahaba wa Mtume (s.a.w.w), moja kati ya masharifu akatoka kuelekea katika ardhi ya Karbala, akakubali aafe ili waislamu wawe kitu kimoja. Lakini si hivyo tu; umoja wa kiwanadamu, umoja wa kiutu ulikuwa umesambaratika kipindi hicho na wakatih uwo.


Imam Hussain (as) katika msafara wake walikwepo waislamu wa madehebu zote na pia watu wasioku wawaislamu.


Alikwepo mtumoja aitwaye John; ambaye sio mwislamu wala sio jina la kiislamu. Kwa hivyo kutoka kwa Imam hussain (as) kulikuwa funzo ya kuleta umoja kwa binadamu wote. Pasipo kuwa na kubagua dini zao, pasina kuangalia rangi zao; ni mabadaliko kwa ajili ya waislamu, ni mabadaliko kwa ajili ya utu na mwandamu. Waislamu, Wakristo, ma Yahudi, ma pagani, hawa wote waliungana na Imam Hussain (as).


Leo hii dunia inahitaji amani. Amani imesambaratika, upendo umesambaratika. Lengo la kutoka kwa matembezi haya kwa ajili ya Imam Hussain (as) nikutaka kunyanua sauti kwamba amani, utlulivu na upendo ni moja ya jambo muhimu na lienziwe na liangaliwe kwa makini.
Jumuiya ya Khoja Shia Ithanasheri ni nini?


Jumuiya hii ya waislamu, Khoja Shia Ithanasheri inatoa misaada nyingi ya kibinadamu na msaada kwa watu wa Tanzania kwa ujumla. Wanaendesha hospitali ya Ebrahim Haji iliyopo katikati mwa mji, ambacho kina bei ya chini sana na huduma bora.


Hivi majuzi pia tulifungua kituo cha macho ambapo wanabei za chini na hufanya shughuli za jicho bure pamoja na kufanya opereshen wa mtoto la jicho (cataract), tupo Temeke karibu na Chuo cha Bandari na hudumia maeneo yaliyozunguka. Pamoja na hili, wanashirikana na ‘damu salama’ kufanikisha zoezi la uchangiaji damu, ambaye wanatarajia kufanya tena ndani ya mwezi huu.

Imetolewa na Bw. Imran Sherali, Katibu wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna’Asheri Dar Es Salaam, Ahamisi Agosti 19,2021

Post a Comment

0 Comments