MBUNGE wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (NGOs Tanzania Bara) na Balozi wa Covid19 Tanzania, Mhe Neema Lugangira akizungumza wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa COVID19 tarehe 12 Agosti 2021
MBUNGE wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (NGOs Tanzania Bara) na Balozi wa Covid19 Tanzania, Mhe Neema Lugangira akizungumza wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa COVID19 tarehe 12 Agosti 2021
MBUNGE wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (NGOs
Tanzania Bara) na Balozi wa Covid19 Tanzania, Mhe Neema Lugangira
amesema Wabunge wana nafasi ya kipekee ya kuweza kuihamasisha jamii kwa
kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kujikinga na Ugonjwa wa COVID19 kupata
Chanjo.
Mbunge Lugangira
aliyasema hayo wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa COVID19 tarehe 12 Agosti
2021 ambapo alisema Wabunge wakipatiwa elimu itakuwa ni rahisi kwao
kuifikisha kwa jamii ikiwemo kuondosha dhana potofu iliyopo miongoni mwa
jamii kuhusu chanjo hizo.
Alisema
upo umuhimu wa Wabunge kupatiwa elimu kwa sababu wana jukumu la kuwa
sehemu ya mafanikio ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan katika mapambano
dhidi ya ugonjwa wa COVID19
“Naomba
nisema wazi kuwa ndio Chanjo ya COVID19 ni hiari lakini kwa nafasi zetu
kama Wabunge hatupaswi kutumia hiari yetu kama kigezo cha kuwafanya
wananchi wasitumie hiari yao na tunatakiwa tuwaelemishe kwa usahihi ili
kila mtu atumie hiari yake ya kupata Chanjo ya COVID19” Alisema kwa
hisia kali.
Hata hivyo
aliwapongeza sana Wabunge wenzake kwa kuwa mstari wa mbele kuchoma
Chanjo ya COVID19 wao wenyewe na kuhamasisha wananchi wa majimbo na
mikoa yao kuchoma Chanjo ya COVID19.
Alisema
kwa niaba yao anaomba moja ya Maazimio ya Mdahalo huo iwe ni kuja na
utaratibu wakuwaelimisha na kuwatumia Wabunge katika mapambano dhidi ya
Ugonjwa wa COVID19 kama inavyofanyika kwa makundi mengine.
Hata
hivyo alisema akiwa kama Mbunge kijana anatoa pongezi nyingi kwa Mhe
Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelekea Chanjo na yeye mwenyewe
kukubali Chanjo ya COVID19, kuchanjwa mubashara huku wananchi na dunia
ikushuhudia kitendo kilichodhihirisha pasi na shaka kuwa Chanjo ya
COVID19 ni salama.
Alisema
kwamba tokea Wimbi la Kwanza la COVID19 hadi sasa Wimbi la Tatu, Kirusi
cha COVID19 kimeshajibadilisha sana na kila kinapojibadilisha kinazidi
kuwa hatari.
Aliongeza
kwamba hali hii ilipelekea dunia kuona njia pekee ya kukabiliana na
Kirusi kinachosababisha Ugonjwa wa COVID19 na kupunguza makali yake hata
pale utakapoipata ni Chanjo ya COVID19.
Hivyo,
kwakuwa Tanzania sio Kisiwa ilikuwa ni muhimu pia wafanye tathmini juu
ya Ugonjwa wa COVID19 na nini kifanyike kama Taifa na kwa mara nyingine
tena na Mbunge Neema Lugangira alimpongeza sana Mhe Rais Samia Suluhu
Hassan kwa Maamuzi Sahihi na Wakati Sahihi wakuleta Chanjo ya COVID19
nchini.
Mara baada ya
kuhitimisha Hotuba yake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto alisimama na kukiri kutambua kazi kubwa ambayo Mbunge
Neema Lugangira amefanya katika kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu
kujikinga na Ugonjwa wa COVID19 tokea Wimbi la Kwanza na hadi katika
Wimbi la Tatu na kuendelea kuemilisha na kuhamasisha jamii kuhusu Chanjo
ya COVID19 hivyo alimteua kuwa Balozi wa COVID19 Tanzania.
0 Comments