Ticker

6/recent/ticker-posts

MHE. MARY MASANJA ASISITIZA WAWEKEZAJI KUWEKEZA KWENYE VIVUTIO VYA UTALII CHATO

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amefunga maonyesho ya Utalii na Biashara Wilayani Chato yaliyoanza Agosti 8 hadi 15,2021.

Akizungumza katika hafla ya kufunga maonyesho hayo Mhe. Masanja ametoa wito kwa wawekezaji kuanza kuwekeza kwenye maeneo ya vivutio vya utalii vilivyoko Chato akitolea mfano wa fukwe za Ziwa Victoria, hifadhi ya kisiwa cha Rubondo na pori la Burigi.

Amesema Serikali inatambua umuhimu wa wawekezaji ndio maana imeanza kuboresha miundombinu ya kuwezesha watalii kufika katika hifadhi hizo ambapo imejenga Uwanja wa Ndege wa Mfugale, hoteli ya nyota tatu na inaendelea kuboresha maeneo mengine ili kuvutia watalii wengi.

Amesema Serikali pia ina mkakati wa kuboresha utalii wa majini kwa kununua boti na inaendelea kuangalia namna ya kuwapata watalii wanaotoka Serengeti, Kisiwa cha Saanane na maeneo mengine kutembelea vivutio vya Chato.

Aidha amewahamasisha watanzania kutangaza vivutio.



Post a Comment

0 Comments