Katika jitihada za Serikali kupambana na dawa za kulevya hadi sasa kuna vituo 11 vyenye waathirika 10,560 wanaolelewa huku hatua za udhibiti wa vipenyo vya dawa hizo zikiimarishwa jitihada zikifanywa na mamlaka husika kwa kushirikiana na jeshi la polisi.
Ameysema hayo leo Jijini dar es Salaam, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana na Ajira) Mhe.Patrobas Katambi
wakati wa mkutano wake na wandishi wa habari, uliolenga kutoa ujumbe wa serikali kwa vijana nchini.
Amesema mpango wa serikali ni kuhakikisha kijana akikosa ajira anapata kazi, kwani kazi zipo nyingi isipokuwa baadhi yao huchagua.
"katika ajira kwa vijana, nyingi zimezalishwa kutokana na utekelezaji wa miradi ya kimkakati. Utoaji wa mikopo inayotokana na mapato ghafi ya halmashauri ambapo hadi sasa zaidi ya sh. bilioni 30 zimetengwa". amesema Mhe.Katambi.
Amesema mambo mengine ni ujenzi wa shule, utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, kugharimia mafunzo ya elimu ya ufundi kwa vijana na kuwajengea uzoefu wa kazi wahitimu wa vyuo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi akizungumza masuala ya vijana na mwelekeo wa Serikali katika kushughulikia masuala yanayohusu vijana wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Agosti 14, 2021 katika Ofisi za PSSSF Jijini Dar es Salaam.
Afisa Kazi Mwandamizi (TAHESA) Bw. Peter Ugata akitoa maelezo ya mipango ya Serikali katika kutoa mafunzo tarajali (internship program) kwa vijana ili saidia kutatua changamoto ya ajira nchini wakati wa mkutano huo.
Afisa Mfawidhi Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Bw. Nashon Mguna akieleza namna ofisi yake inavyotekeleza majukumu yake katika kulifikia kundi la vijana na changamoto za migogoro sehemu za kazi wakati wa mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda akizungumza kuhusu masuala ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi wakati wa mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Habari Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Bw.Jumanne Isango akitoa ufafanuzi juu ya mikakati ya Serikali kuendelea na mapambano dhidi ya UKIMWI nchini wakati wa mkutano huo.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
0 Comments