Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), (hawapo pichani) mara baada ya kufika katika ofisi za shirika hilo zilizopo Wilaya ya Kigamboni Mkoani Dar es Salaam na kutaka shirika hilo kujiendesha kibiashara na kuwa na mpango kazi wa kuhakikisha linaleta tija kwa wavuvi wadogo. (10.08.2021)
Kaimu Meneja Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) Bi. Esther Mndeme akifafanua kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega juu ya ukarabati wa miundombinu iliyopo katika ofisi hizo zilizopo Wilaya ya Kigamboni Mkoani Dar es Salaam na kuishukuru wizara namna ambavyo inaendelea kutoa fedha kuhakikisha ukarabati unafanyika kwa wakati na shirika kuanza rasmi kutumia miundombinu hiyo. (10.08.2021)
Picha ya pamoja ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) na wafanyakazi wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), mara baada ya Naibu Waziri Ulega kufika katika ofisi hizo zilizopo Wilaya ya Kigamboni Mkoani Dar es Salaam kushuhudia ukarabati wa miundombinu unaoendelea kufanywa katika jitihada za kufufua shirika hilo. (10.08.2021)
0 Comments