Ticker

6/recent/ticker-posts

RC MAKALLA AAGIZA KUKAMATWA MKURUGENZI WA KAMPUNII YA GEOLINK SOLUTION TANZANIA LTD

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amevielekeza vyombo vya dola kumkamata Mkurugenzi wa Kampuni ya Upimaji wa Ardhi ya Geolink Solution Tanzania LTD kwa tuhuma za kukusanya fedha za Wananchi zaidi ya Shilingi Milioni 18 wa eneo la Mtaa wa Mbezi Kati kwaajili ya zoezi la Upimaji wa Ardhi na kuingia mitini.RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara ya kusikiliza Migogoro Jimbo la Kawe ambapo ameelekeza pia kampuni zote zilizochukuwa fedha za Wananchi na kuingia mitini wahusika wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kero ya Wananchi hao zaidi ya 100 wa eneo la Maendeleo mtaa wa Mbezi Kati limeibuliwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo aliejumikana kwa majina ya Frank Mwanga.

Post a Comment

0 Comments