Ticker

6/recent/ticker-posts

TBL PLC YANG’ARA MAKAMPUNI YENYE MTAJI MKUBWA AFRIKA MASHARIKI



Waziri wa Viwanda na Biashara,Profesa Kitila Mkumbo, (kushoto) akiangalia mifumo ya uzalishaji ya TBL, alipotembelea kiwanda cha bia cha Dar es Salaam hivi karibuni.

Mkurugenzi wa TBL, Jose Moran, akieleza shughuli za kampuni kwa Wabunge wa Kamati ya Viwanda walipotembelea kiwanda cha Ilala

Waziri wa Uwekezaji Geofrey Mwambe akitoa hotuba wakati wa hafla ya uzinduzi wa ripoti ya mchango wa TBL katika kukuza uchumi nchini iliyofanyika jijini Dar es Salaam
***


Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL Plc) imeendelea kushikilia rekodi ya kuwa miongoni mwa makampuni yaliyoorodheshwa kwenye Masoko ya Hisa, yanayoongoza kwa kuwa na mtaji mkubwa katika kanda ya Afrika mashariki.


Kwa mujibu wa ripoti ya Jarida ya African Business ya hivi karibuni ambayo inachambua utendaji wa makampuni makubwa yaliyoorodhesha, imebainisha kuwa TBL ni kampuni ya 2 kwa kuwa na mtaji wa soko katika Afrika Mashariki, ikitanguliwa na kampuni ya mawasiliano ya Safaricom ya nchini Kenya.


Kwa zaidi ya miaka 15,Jarida la African Business la nchini Uingereza hutoa orodha ya makampuni yaliyoorodheshwa 250 yenye mtaji mkubwa barani Afrika ambapo ripoti ya karibuni imeorodhesha mataifa 18 yaliyofanikiwa kutoa kampuni hizo huku Afrika Mashariki ikichangia kampuni 20.


Makampuni ya Afrika Mashariki yalichaguliwa kupitia utendaji wake katika Soko la Hisa la Nairobi,Soko la Hisa la Dar es Salaam na Soko la Hisa la Uganda.


Jarida la Africa Business limebainisha kuwa mtaji wa TBL ni dola bilioni 1.4 ambapo mbali na kushikilia nafasi ya pili Afrika Mashariki inashilia nafasi ya 90 Afrika, na kampuni inayoongoza ya Safaricom ina mtaji unaofikia dola bilioni 13.3 za kimarekani na inashikilia nafasi ya tisa kwa upande wa Afrika.


Makampuni mengine kutoka Afrika yaliyoorodheshwa na jarida hilo ni Equity (Kenya) mtaji wa dola bilioni 1.3,KCB (Kenya) mtaji wa dola bilioni 1.2,EABL mtaji wa dola bilioni 1.1,Vodacom (Tanzania) dola milioni 744,TCC (Tanzania) dola milioni 733,Co-op Bank (Kenya) dola milioni 708,NMB (Tanzania) dola 505, na StanChart (Kenya),dola milioni 490

Post a Comment

0 Comments