Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) amewataka wajumbe wa bodi ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo (TEMDO) kufanya kazi kwa weledi na kulinda maslahi ya umma kwani taasisi hiyo ilianzishwa kwa madhumuni ya kufanya kazi ya kutafiti, kubuni, kuunda na kuendeleza teknolojia.
Mhe. Mkumbo ameyasema leo tarehe 10 Agosti, 2021 alipokuwa akizindua Bodi ya wakurugenzi ya TEMDO na kueleza kuwa bodi ndio mhimili wa ukuaji wa taasisi kwani wao ndio watakuwa wanaisimamia taasisi na kuishauri serikali juu ya nini kifanyike kuhakikisha malengo na mikakati iliyowekwa inafikiwa.
Mhe. Mkumbo amempongeza Mwenyekiti wa bodi hiyo Dkt. Richard Masika kwa kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye amempa jukumu la kuisimamia bodi hiyo.
Mhe. Mkumbo ameitaka TEMDO kujikita Zaidi katika utafutaji wa masoko ya teknolojia wanazozibuni, kushirikiana na wajasiriamali kwa kuwapa huduma bora za mahitaji yao hivyo basi ni vyema TEMDO ikawa na vipaumbele vichache vyenye tija na hivyo kuihaidi kuisaidia kupata fedha kwa ajili ya kuimarisha utafiti wa teknolojia mbalimbali.
Naye, Naibu waziri Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) amesema kuwa TEMDO ni taasisi muhimu sana katika nchi hii ukizingatia ile zana ya ujenzi wa Viwanda inachagizwa na ubunifu wa teknolojia.
Awali Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil T. Abdallah, kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wizara ya Viwanda na Biashara, alitumia fursa hiyo kutambulisha bodi hiyo kwa mgeni rasmi ambaye ni waziri wa viwanda na baadaye, na baada ya utambulisho wa bodi Mwenyeiti wa kamati hiyo Dkt. Richard Masika alikula kiapo cha maadili ya uongozi wa Umma.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akizungumza mara baada ya kuwasili katika ofisi za TEMDO mkoani Arusha kwaajili ya kuzindua Bodi ya wakurugenzi ya TEMDO.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TEMDO Prof. Frederick Kahimba pamoja na mwenyekiti wa bodi ya TEMDO Dkt. Richard Masika, mara baada ya kuwasili katika ofisi za TEMDO mkoani Arusha.
Mwenyekiti wa bodi ya TEMDO Dkt. Richard Masika akizungumza mara baada ya kuapa kiapo Cha uadilifu kuiongoza bodi hiyo.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na bodi ya wakurugenzi ya TEMDO mara baada ya uzinduzi.
0 Comments