Ticker

6/recent/ticker-posts

UJENZI WA KITUO CHA KIMATAIFA CHA BIASHARA NCHINI KUKAMILIKA JUNI 2022


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EPZA Bw.John Mnali (katikati) akiwa pamoja na Meneja wa Mradi BICO, Mhandisi Lwitiko Kalenga (wa kwanza kulia) wakitia saini wa mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa kituo cha kimataifa cha biashara leo Kurasini Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akizungumza wakati utiaji saini wa mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa kituo cha kimataifa cha biashara, ukiwemo makabidhiano ya eneo kwa ajili ya ujenzi wa ukuta kati ya Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA) na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA-JKT) leo Kurasini Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EPZA Bw.John Mnali akizungumza wakati utiaji saini wa mikataba miwili ya ujenzi wa mradi wa kituo cha kimataifa cha biashara, ukiwemo makabidhiano ya eneo kwa ajili ya ujenzi wa ukuta kati ya Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA) na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA-JKT) leo Kurasini Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*******************************

Serikali imeweka wazi kukamilisha ujenzi wa kituo cha kimataifa cha biashara na lojistiki Kurasini Jijini Dar es Salaam ambapo pia kutakuwepo na huduma nyingine nyingi (One stop Service center) ambazo zitamuwezesha mfanyabiashara kupata huduma karibu na haraka.

Ameyasema hayo leo Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo wakati akishuhudia utiaji saini wa mikataba miwili ya ujenzi wa mradi huo, ukiwemo makabidhiano ya eneo kwa ajili ya ujenzi wa ukuta kati ya Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA) na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA-JKT).

Mkataba mwingine ni kati ya EPZA na Mhandisi Mshauri wa mradi huo ambayo ni kampuni ya BICO ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kwa ajili ya upembuzi yakinifu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Prof. Mkumbo amesema hadi kufikia Juni mwakani mradi huo unatarajiwa kukamilika ambapo Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania anatarajia kuzindua ujenzi huo kufikia mwezi Februari 2022.

Amesema tayari serikali imeshatoa sh. bilioni 30 kwa ajili ya hatua za awali za utekelezaji wa mradi huo, zikihusisha ujenzi wa ukuta na upembuzi yakinifu, ujenzi wa miundombinu wezeshi ukiwemo umeme na maji.

Aidha amesema mradi huo utatekelezwa kwa ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi ambapo tayari wawekezaji watano kutoka sekta binafsi wameshapatikana.

Pamoja na hayo ameitaka SUMA JKT kuhakikisha inakamilisha kazi ya ujenzi wa ukuta huo Januari mwakani, huku upembuzi yakinifu utakaofanywa na kampuni ya BICO ukamilike mwishoni mwa mwaka huu.

“Hiki kitakuwa kituo cha kwanza kujengwa nchini, tangu Rais Samia Suluhu Hassan, alipohotubia kuonyesha dhamira yake ya kuejnga vituo hivi na ikimpendeza huu tutauita Samia Industrial Park,” alisema.

Hata hivyo amesema chimbuko la mradi huo ni Kikao kati ya China na Tanzania kilichofanyika Misri na kuchagua nchi nne ikiwemo Tanzaniazitakazojengwa vituo vya kimataifa vya biashara na Lojistiki.

Post a Comment

0 Comments