Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN KUHUDHURIA MKUTANO WA COP 26 UTAKAOFANYIKA GLASGOW, SCOTLAND*******************************

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kesho tarehe 30 Oktoba, 2021 anatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Glasgow, Scotland kuhudhuria Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26).

Pamoja na mambo mengine yatakayojadiliwa katika Mkutano huo wa COP 26, Mhe. Rais Samia anatarajiwa kuhutubia siku ya pili ya Mkutano huo tarehe 02 Novemba, 2021.

Aidha, Mhe. Rais Samia anatarajiwa pia kukutana na kuzungumza na baadhi Wakuu wa nchi, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa, Wakuu wa Taasisi mbalimbali pamoja na wafanyabiashara wakubwa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya Tanzania na nchi hizo pamoja na Taasisi zao.

Lengo la Mkutano huo wa COP 26 ni kujadili jitihada za kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa ili kupunguza joto duniani.Jackson Msangula

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Post a Comment

0 Comments