Ticker

6/recent/ticker-posts

RC MAKALLA ATAKA USHIRIKISHWAJI WA VIJANA WA SCOUT KWENYE MATUKIO MBALIMBALI DSM.*******************************

- Asema umuhimu wao usionekane wakati wa Matukio ya majanga na Mikutano pekee.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amemuelekeza Afisa Elimu wa Mkoa huo kuhakikisha kuanzia Sasa Vijana wa Scout wanashirikishwa Katika shughuli mbalimbali na sio kusubiri yatokee Matukio ya Majanga, Mikutano, ugeni wa Viongozi au Misiba ndipo umuhimu wao unaonekana.


RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati alipotembelewa ofisini kwake na Kamishina wa Scout Dar es salaam alieambatana na Watendaji wa TAKUKURU na kukabidhiwa Kitabu Cha Mwongozo wa mafunzo kwa wawezeshaji kufundisha Vijana wa Scout kuhusu kuzuia na kupambana na Rushwa.

Post a Comment

0 Comments