Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAJIPANGA KUTOA ELIMU KWA WAGONJWA KABLA YA KUFANYA WARD ROUND



******************

Na.WAMJW-Iringa

Serikali ya Tanzania inawajali wananchi wake kwa kuwaletea chanjo mbalimbali kwani tangu awali imekua ikifanya hivyo ili kuondoa magonjwa mbalimbali ikiwemo tetenasi na magonjwa mengine yanayokingwa kwa chanjo ambayo yamekuwa yakiwathiri binadanu wakiwemo watoto chini ya miaka mitano. 




Hayo yamesemwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa Dkt. Alfred Mwakalebela wakati akiongea kwenye ofisi yake ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa jamii Shirikishi na Harakishi dhidi ya chanjo ya UVIKO-19 ambao unaratibiwa na Wizara ya afya na TAMISEMI.




Dkt. Mwakalebela amesema kuwa yapo magonjwa mengi ambayo yanakingwa kwa chanjo na ameongeza kuwa hata zamani watu wengi walikuwa wanakufa na matatizo lakini Serikali kwa kuwajali wananchi wake ikaamua kuleta chanjo .




“Mfano huko nyuma kulikuwa na makabila yakitoboa meno ya mbele kwa ajili ya kumlisha mtu endapo ataugua tetenasi, lakini yote hayo yameondoka kutokana na chanjo, hata ugonjwa wa Surua naye imeondolewa kwa chanjo”. Alisisitiza.




Katika utekelezaji wa Mpango wa Jamii Shirikishi amesema hospitali yake wamejipanga kutoa elimu kwa wagonjwa kabla ya kufanya ‘ward round’, kwenye famasi, kliniki zote zilizopo kwenye hospitali hiyo pamoja na sehemu ya kungojelea (mapumziko) ambapo ndugu wa wagonjwa hukaa hapo na kupatiwa elimu ya chanjo dhidi ya UVIKO-19.




Dkt. Mwakalebela amesema kuwa watu wengi hivi sasa wanaelewa umuhimu wa chanjo hiyo muitikio kwa wakazi wa mji wa iringa umekuwa mkubwa na hivyo wanajitokeza kwa wingi kila siku.

Post a Comment

0 Comments