Ticker

6/recent/ticker-posts

VIONGOZI WA SKIMU ZA UMWAGILIAJI WATAKIWA KUSIMAMIA UKUSANYAJI WA ADA NA TOZO.

Mhandisi Umwagiliaji Mkoa wa Iringa Bw. Onesmo Kahoggo akingumza kuhusu Viongozi wa skimu za kilimo cha Umwagiliaji Nchini, kusimamia ukusanyaji wa ada na Tozo za Umwagiliaji.

Bi Katarina Rashid Mlaga, mkulima mkazi wa kijiji cha Mgozi akiishuru Serikali kwa kurejesha mto Ruaha Mdogo katika njia yake ya asili.

Picha Ikionesha mto Ruaha mdogo baada ya kurejeshwa katika njia yake ya asili.

Picha ikionesha Roli la kubebea mchanga likiwa kazini wakati wa ukarabati wa mto Ruaha mdogo.


**************************


Na; Mwandishi Wetu – Pawaga Iringa.

Mhandisi wa Umwagiliaji Mkoa wa Iringa Onesmo Kahoggo amewataka viongozi katika Skimu za Umwagiliaji kusimamia kikamilifu zoezi la ukusanyaji ada na tozo kwa lengo la kutunisha mfuko wa Umwagiliaji.

Akizungumza mjini Iringa Bw, Kahoggo amesema endapo wakulima katika Skimu za Umwagiliaji watachangia fedha za ada ya usajili na matunzo kwa wakati, itasaidia kuharakisha ukarabati wa Skimu zilizoharibika kutokana na athari zitokanazo na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kujenga Skimu mpya nchini.

Ametolea mfano zoezi la kuurejesha mto Ruaha Mdogo katika njia yake ya asili limegharimu fedha kutoka mfuko wa Umwagiliaji ambao unahitaji kuwezeshwa na wakulima hao.

Kwa upande wake Bi, Katarina Rashidi Mlaga mkulima mkazi wa kijiji cha Magozi ameishukuru serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa kazi kubwa iliyofanya wa kurejesha mto Ruaha Mdogo katika njia yake ya asili, nakusema kuwa wakulima katika kijiji hicho hutegemea Zaidi kilimo cha umwagiliaji, na wamepata elimu ya kutosha kuhusu uchangiaji wa tozo za umwagiliaji na wapo tayari kuchangia.

Awali akiongea kijijini hapo Diwani wa kata ya Ilolo Mpya Bw, Funda Mihayo amemshukuru Mkurugenzi wa Tume ya taifa ya Umwagiliaji Bw, Daudi Kaali kwa kuwezesha wataalam wa tume kurekebisha miundombinu ya mifereji ya kupeleka maji katika mashamba ya wakulima pamoja na zoezi la usanifu linaloendelea katika Skimu ya Liganga ambapo lengo ni kuwezesha maji kunyweshea Skimu ya Magozi na Mkombilenga.

Post a Comment

0 Comments