Ticker

6/recent/ticker-posts

VODACOM TANZANIA FOUNDATION YAWAJENGEA UWEZO WA TEHAMA WASICHANA WILAYANI KISARAWE


Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Vodacom Tanzania Jacquiline Materu (wa pili kulia) akimueleza jambo Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe Mwanana Msumi (wa pili kushoto) baada ya Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kutoa kompyuta 15, TV, Router na samani kwa shule ya wasichana ya Jokate Mwegelo iliyopo wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ikiwa na lengo la kuhakikisha wanafunzi wanapata maudhui ya elimu bure kupitia tovuti ya e-fahamu. Kulia ni Mtaalamu wa mifumo ya kompyuta Vodacom Tanzania Plc (kulia) na Afisa Elimu wilaya ya Kisarawe Alice Nkwera.


Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe Mwanana Msumi akimkabidhi moja ya kompyuta zilizotolewa na Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa Afisa Elimu wa wiliaya hiyo Alice Nkwera. Vodacom Tanzania Foundation ilitoa kompyuta 15, TV, Router na samani kwa shule ya wasichana ya Jokate Mwegelo iliyopo wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ikiwa na lengo la kuhakikisha wanafunzi wanapata maudhui ya elimu bure kupitia tovuti ya e-fahamu. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Vodacom Tanzania Jacquiline Materu (kulia) na Mkuu wa Shule ya Jokate Mwegelo Mariam Mpunga (kushoto).
Mtaalamu wa mifumo ya kompyuta Vodacom Tanzania Plc Omari Amiri akionyesha utaalamu wa kompyuta kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe Mwanana Msumi (wa pili kushoto) baada ya Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kutoa kompyuta 15, TV, Router na samani kwa shule ya wasichana ya Jokate Mwegelo iliyopo wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ikiwa na lengo la kuhakikisha wanafunzi wanapata maudhui ya elimu bure kupitia tovuti ya e-fahamu. Wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Vodacom Tanzania Jacquiline Materu na kushoto ni Afisa Elimu wilaya ya Kisarawe Alice Nkwera.

**************************

• Vodacom Tanzania Foundation yatoa mchango wa vifaa vya kompyuta na samani kwa shule ya Sekondari ya Wasichana Jokate Mwegelo.



• Vifaa vilivyokabidhiwa vina thamani ya Sh. Milioni 38, zikiwemo kompyuta 15, TV, Router na samani.

• Mchango unalenga kujenga ushirikishwaji katika elimu kwa kujenga uwezo wa TEHAMA kwa wanafunzi wa kike na waalimu ili kujenga tabia bora za kujifunza na kujisomea.







Kisarawe. Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania Foundation leo imekabidhi mchango wa vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa shule ya sekondari ya Wasichana Jokate Mwegelo iliyoko wilayani Kisarawe.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya Shilingi milioni 37,856,170 vimekabidhiwa na Mkurugenzi wa taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation Bi Rosalynn Mworia katika hafla iliyofanyika viwanja vya shule hiyo, huku vifaa hivyo vikitegemewa kuwanufaisha wanafunzi 150 wanaosoma katika shule hiyo.

Akiongea wakati wa hafla hiyo Bi. Mworia alisema, “Tunafanya hivi kwa lengo la kujenga jamii jumuishi na isiyo tenga baadhi ya watu wake kwa sababu za kijinsia, uwezo, kiuchumi wala ulemavu, tukiamini kwamba kila mmoja wetu ana nafasi yake katika jamii, ana mchango wake kwa maendeleo ya jamii zetu na taifa na pia kila mmoja wetu anastahili kunufaika na matunda ya maendeleo yanayopatikana nchini mwetu.”




Vifaa vilivyokabidhiwa ni kompyuta 15, viti 15, meza 15, TV moja ya inchi 65 na kipanga njia (Router) Mchango huu unalenga kusaidia waalimu kuweza kutoa mafunzo bora ya TEHAMA na kwa wanafunzi kuweza kujenga tabia njema za kujisomea pamoja na kujiamini kutokana na stadi za kiteknolojia watakazozipata.




Akipokea msaada huo, kwa niaba ya shule, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Bw. Nixon Simon aliishukuru taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, huku akiongeza kwamba, “Wilaya ya Kisarawe imekuwa ikijitahidi kupambana na changamoto mbalimbali zinazosababisha wanafunzi waende nje ya maeneo yao kutafuta elimu kama hii ya TEHAMA, Kufuatia mchango huu, tunaamini kuwa tutakuwa na uwezo wa kutoa huduma hii muhimu kwa walengwa wetu hapa hapa Kisarawe. Tunashukuru kwani sasa elimu hii itakuwa inawafikia wanafunzi wetu wakiwa hapa hapa, hawana tena haja ya kwenda mbali.”




Vodacom Tanzania Foundation, imekabidhi msaada wake wilayani Kisarawe ikiwa ni muendelezo wa mkakati maalum wa kuwaongezea Wasichana uwezo katika fani za Hisabati, Sayansi na TEHAMA.




Akifafanua zaidi, Mworia alisema, “Katika malengo makuu ya Vodacom Tanzania Foundation, ni kuwajengea uwezo wasichana na wanawake katika nyanja za elimu, afya, uchumi na kijamii kwa jumla. Mchango wetu siku ya leo unaendana na dhamira yetu ya kusaidia wasichana na pia kushirikiana na serikali katika kujenga jamii iliyoelimika.”




Vodacom Tanzania Foundation imekuwa ni mshirika mkubwa wa serikali kwa kutoa mchango mkubwa wa vifaa vya elimu, ambapo mpaka sasa taasisi hiyo imeshatoa kompyuta zaidi ya 800 kwa shule 187 zilizoko katika mikoa 30 nchini, huku mradi wake wa E-Fahamu ukiwafikia wanafunzi zaidi ya 180,000 nchi nzima.

Post a Comment

0 Comments