Ticker

6/recent/ticker-posts

BALOZI TOGOLANI MAVURA AWASILISHA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO KWA NAIBU WAZIRI NA MKUU WA ITIFAKI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE YA JAMHURI YA KOREA

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jamhuri ya Korea, Mhe. Togolani Edriss Mavura, leo tarehe 30 Novemba 2021 amewasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Naibu Waziri na Mkuu wa Itifaki Balozi Jeongyun RYU wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea jijini Seoul.


Akiongea baada ya kupokea Nakala hizo, Balozi Ryu amempongeza Balozi Mavura kwa imani kubwa aliyopewa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kumuwakilisha nchini humo.


Pia ametumia nafasi hiyo kumhakikishia utayari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Serikali ya Korea kwa ujumla kumpatia ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake ikiwemo kuimarisha ushirikiano na uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Korea.


Naye Balozi Mavura alimshukuru Balozi Ryu kwa mapokezi mazuri aliyopata kutoka Serikali ya Korea tangia alipowasili nchini Korea tarehe Novemba 10, 2021, na kutenga muda wake kupokea Nakala za Utambulisho.


Aidha, Balozi Mavura alielezea kufurahishwa kwa hali ya uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Korea unaoelekea kutimiza miaka 30 mwezi Aprili 2022.


Vilevile, Alimfahamisha mwenyeji wake juu ya azma yake ya kuuona ushirikiano huu unazidi kuimarika siku za usoni kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na Korea.Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jamhuri ya Korea, Mhe. Togolani Edriss Mavura, leo tarehe 30 Novemba 2021 amewasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Naibu Waziri na Mkuu wa Itifaki, Balozi Jeongyun RYU wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea jijini Seoul.


Makabidhiano yakiendelea, wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi wa Tanzania katika jamhuri ya Korea, Bw. Deogratius Mwanyasi akishuhudia makabidhiano hayo.

Post a Comment

0 Comments