Ticker

6/recent/ticker-posts

ENDELEENI KUWA WAADILIFU NA WACHAPA KAZI KATIKA KUWAHUDUMIA WAGONJWA - DKT. GWAJIMA.


*******************************

Na Rayson Mwaisemba, WAMJW-Mwanza.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo ametoa wito kwa Wataalamu wa Radiolojia nchini kuendelea kuchapa kazi kwa kufuata maadili na taratibu za taaluma yao ili wananchi waendelee kunufaika na huduma hiyo.

Dkt. Gwajima ametoa wito huo leo wakati akifunga Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Tara uliofanyika Jijini Mwanza wenye ujumbe usemao "Jukumu la Radiographa katika janga la UVIKO-19. "

Amesema taaluma hii ya Radiographa inamchango mkubwa katika Sekta ya afya, hivyo ni muhimu kwa Wataalamu hao kutoa huduma kwa usawa, usalama na kwa ubora wa hali ya juu ili kuwatosheleza wananchi wa hali zote.

"Endeeni kuwa waaminifu na wachapa kazi mkiwasaidia wagonjwa mnaowahudumia kwa usawa, usalama na kwa ubora wa hali ya juu" Amesema Dkt. Gwajima.

Aidha, Dkt. Gwajima amempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha hospitali zinapata mashine za Ultrasound 125, Digital X-ray 108, CT Scan 29 na MRI 4 kabla ya Juni, 2022 kupitia mpango wa Maendeleo na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Mbali na hayo Dkt. Gwajima amesema, mwa mwaka 2020/2021, Serikali kupitia Wizara ya Afya imeweza kuajiri Rediographa 46 ambapo Rediographa 16 wameajiriwa kwaajili ya hospitali za Rufaa za Mikoa na Rediographa 30 kwaajili ya hospitali zilizo chini ya TAMISEMI.

"Kwa upande wa ajira ya Wateknolojia mionzi kwa mwaka 2020/2021, Serikali kupitia Wizara ya Afya imeweza kuajiri Radiographa 46 ambapo 16 wameajiriwa kwa ajili ya hospitali za Rufaa za Mikoa na 30 kwa ajili ya hospitali zilizo chini ya TAMISEMI." Amesema.

Hata hivyo, ameeleza kuwa, Serikali imeendelea kuboresha hospitali za Rufaa za Mikoa 28 kwa kuzipatia mashine mpya za kisasa za X-ray na kuhakikisha huduma hizi zinapatikana kwa zaidi ya asilimia 90% kwa gharama nafuu na kwa ubora unaotakiwa.

Mbali na hayo, amesema Serikali imeendelea kuboresha huduma za mionzi katika hospitali ya Taifa maalumu na kanda ili kupunguza rufaa za nje ya nchi, huku akisisitiza kuwa, mashine hizo zimesaidia kuboresha ubora wa matokeo ya uchunguzi na kuimarisha matibabu yakibingwa nchini.

"Serikali imeendelea kuboresha huduma za mionzi katika hospitali ya Taifa maalumu na kanda ili kupunguza rufaa za nje ya nchi. Mashine hizo zimesaidia kuboresha ubora wa matokeo ya uchunguzi na kuimarisha matibabu yakibingwa." Amesema.

Post a Comment

0 Comments