Ticker

6/recent/ticker-posts

NEMC YATOA TAHADHARI KWA JAMII INAYOFANYA SHUGHULI ZAO KATIKA MAENEO YA VYANZO VYA MAJI

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Mhandisi Dkt. Samuel Gwamaka akisisitiza jambo mbele waandishi wa habari leo katika Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Mhandisi Dkt. Samuel Gwamaka akisisitiza jambo mbele waandishi wa habari leo katika Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Mhandisi Dkt. Samuel Gwamaka akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ofisi za NEMC Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

******************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi, sehemu kubwa shughuli za kibinadamu zimechangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa ukosefu wa maji kwenye vyanzo vya maji katika maeneo mengi ya nchi.

Ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Mhandisi Dkt. Samuel Gwamaka alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari.

Amesema Sehemu kubwa ya vyanzo vya maji ambavyo vimeharibiwa mpaka kuleta upungufu wa maji ni kwasababu ya wananchi na jamii kukosa elimu ya kutosha ya utunzajji wa mazingira na kupelekea kuharibu mazingira pasipokufahamu madhara yake.

"Sehemu nyingi ukiangalia utakuta kuna makolongo, mmomonyoko mkubwa wa ardhi ni kwasababu sehemu kikubwa uoto umeondoka na matokeo yake yale maeneo ambayo yalipaswa kuhifadhi maji kwenye miamba yanazidi kupungua siku hadi siku". Amesema

Aidha amesema kumekuwa na jamii kuvamia maeneo ambayo yangetakiwa kutunza maji na kujenga shughuli zao mwisho wanapeleka kukosekana na chemchem za maji katika maeneo mengi.

"Sasa hivi kuna tabia ya kuanzisha miji hovyohovyo , unaanzisha mji wakati mwingine kwenye maeneo uovu eneo ambalo linapaswa kuwa eneo la asili ambalo linatakiwa kutunza maji. Na sheria ipo inasema kabla haujaanza kujjenga mji lazima ufanye tasmini ya kimkakati ya mazingira". Amesema

Pamoja na hayo amesema ni muhimu kushirikiana pamoja na wenyeviti wa mtaa kuhakikisha vyanzo vya maji vinakuwa salama ili kuondokana na athari za mazingira kwenye vyanzo hivyo.

Post a Comment

0 Comments