Ticker

6/recent/ticker-posts

RC MKIRIKITI AMEITAKA TANROADS KUTENGENEZA NISHANI KWA WADAU WA USAFIRISHAJI

******************

NA MWANDISHI WETU, RUKWA 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe.Joseph Mkirikiti amewataka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kutengeneza nishani kwa wadau makubwa wa usafirishaji hasa wamiliki wa malori kwani ndio wamekuwa watekelezaji wakubwa wa sheria ipasavyo.


Ameyasema hayo leo wakati wa mafunzo kwa wadau wa sekta ya usafirishaji yaliyoandaliwa na (TANROADS) mkoani Rukwa.


“Tunapopeana hizi elimu tutambuane pia wale wanaozingatia sheria na kama inafaa basi tuwape tuzo na hivyo hivyo hata kwa ngazi ya watendaji wetu wa mizani, nao lazima tujue nani anafanya kwa mujibu wa sheria”. Amesema RC Mkirikiti. 


Amesema kuwachagua wao kuwa wenyeji wa mafunzo hayo ni jambo la fahari kwa sababu Mkoa huo unafunguka kwa pande zote na iwapo Mkoa huo utatumika vizuri utakuwa lango la bidhaa zinazotoka Congo.


Aidha RC Mkirikiti amesema kujipanga kimkakati katika utunzaji wa miundombinu ya barabara, kunalenga kupandisha pato la Mkoa huo na taifa, kwa kiwango kikubwa ni miundombinu iliyotunzwa vizuri ndio inawasaidia kusafirisha bidhaa kupeleka sokoni na kukuza pato.

Post a Comment

0 Comments