****************************
NA Richard Mrusha
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Dkt Dorothy Gwajima amewaagiza Wakuu wa Wilaya zote Nchini kufuatilia mienendo ya watumishi wa Afya katika Hospitali Vituo vya Afya na Zahanati wanaokiuka sheria za nchi na utaratibu wa utumishi wa umma kwa kuwatoza wakina mama wajawazito kwa kuwauzia kadi za kliniki kati ya shilingi 2000 hadi shilingi 5000 ili watakaobainika wachukuliwe hatua za kisheria.
Amebainisha hayo wakati akizindua mpango maalumu wa utekelezaji wa watoto wachanga Nest 360 katika hospital ya Rufaa Mkoa wa Temeke Jijini Dar es salaam ambayo imeboresha huduma kwa kuhudumia watoto kutoka watoto 20 Mwaka 2019 hadi kufikia watoto 70 mwaka 2021 kwa siku hali iliyopunguza msongamano katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Aidha Dkt Gwajima Ametoa siku saba kwa hospitali zote nchini kuonyesha taarifa ya utekelezaji wa mpango maalumu watoto wachanga Nest 360 kwa lengo la kupunguza vifo vya watoto wachanga wanaopoteza maisha kwa sababu zisizo zuilika ili kuwa na taifa lenye afya njema
Awali akitoa taarifa za utafiti Mkurugenzi wa Taasisi ya Afya Ifakara Dkt Honorati Masanja amesema kuwa takwimu zinaonyesha zaidi ya watoto wachanga milioni
Moja kusini mwa jangwa la sahara wanafariki Dunia kila mwaka ambapo tanzania hupoteza watoto wachanga 50,000 kila mwaka kwa sababu zinazozuilika
Amesema kuwa kufatia hali hiyo viongozi wa Dunia wamedhamiria kutokomeza vifo vya watoto wachanga kwa asilimia 50 katika uboreshaji wa huduma za Afya Kwenye Hospitali Vituo vya Afya na Zahanati kipitia utekelezaji wa mpango maalumu wa watoto wachanga Nest 360 unaoshirikisha wadau wa taasisi mbalimbali za kimataifa.
0 Comments