Ticker

6/recent/ticker-posts

HALMASHAURI ITOE MIKOPO KWA VIKUNDI VINAVYOLIMA MWANI- PROF.SHEMDOE


********************

Nteghenjwa Hosseah, Mafia

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe ameuelekeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia kuhakikisha wanaviwezesha vikundi vya Wanawake wanaojishughulisha na Kilimo cha mwani Wilayani humo.

Prof. Shemdoe ametoa agizo hilo wakati alipotembelea visiwa na Chole na Juwani kujionea bidhaa mimea bahari inayopatikana katika visiwa hivyo.

Amesema Halmashauri iangalia namna bora ya kuwawezesha wanawake wanaojishughulisha na Kilimo cha Mwani ilo waweze kulima kisasa na kujiimarisha kiuchumi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Eng. Martini Ntemo amesema “zao la mwani linaendelea kupata umaarufu duniani na uhitaji wake ni mkubwa sana hivyo tunaendelea kuwawezesha wakulima wetu kulima kisasa ili waweze kupata soko kwa urahisi.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mwl. Kassim Ndimbo amesema walishaanza kuwawezesha mikopo midogo kwa ajili ya kuimarisha kilimo hicho na sasa mwa Maelekzo hayo ya Katibu Mkui watatoa mikopo mikubwa zaidi kwa vikundi hivyo.

Zao la Mwani hulimwa kando kando ya bahari na wengi wanaojishughulisha na zao hilo ni Wananwake.

Post a Comment

0 Comments