Ticker

6/recent/ticker-posts

MAFANIKIO YA MIAKA SITINI YA UHURU KATIKA SEKTA YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

Kuhusu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji;

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Sera ya umwagiliaji ya Taifa ya Mwaka 2010, ilitoa Mwongozo wa kuwepo kwa mambo mahususi kwenye uendelezwaji wa sekta ya Umwagiliaji pamoja na mambo mengine ni kuwa na chombo cha kuboresha na kusimamia sekta ya umwagiliaji nchini.

Kilimo cha umwagiliaji kilianzia mkoani Arusha enzi za ukoloni, na baada ya Uhuru serikali iliendeleza mikakati mbalimbali ndipo mipango mahuhusi ilianzishwa chini ya wizara husika kama Wizara ya maji na kilimo. Ameeleza Bwana Daudi Kaali, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

Akiongea Ofisini kwake Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Bw. Godwin Mutahangarwa, alisema katika kutekeleza Sera ya Taifa ya Umwagiiaji, ambayo ilitoa muelekeo wa sekta ya umwagiliaji nchini, serikali ilipeleka mapendekezo bungeni ya kuwa na sheria inayoitwa Sheria ya Taifa ya Uanzishwaji wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji. National Irrigation Act ya mwaka 2013.

Imeelezwa kuwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeanza kutekeleza majukumu yake mwaka 2015, ikiwa ni pamoja na uendelezwaji utekelezwaji na kutoa utaalam na kuratibu na kuthibiti shughuli zote za umwagilaji nchini.

Tume imekuwa ikitekeleza sheria na miongozo na kanuni pamoja na kutoa elimu ya sheria hiyo kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Mkurugenzi wa Tume ya taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali anabainisha kuwa Tume ina mpango wa kuanza kutoa elimu kwa wananchi ya namna bora ya kuvuna maji ya mvua kwa ajili kilimo cha umwagiliaji na matumizi mengine.

Anaongeza kuwa kwa kusema kuwa lengo ni kuwawezesha wakulima watumie teknolojia ambazo zitawezesha matumizi madogo ya maji ikilinganishwa na sasa ambapo bado wakulima wengi wanatumia mbinu za kizamani.

MABADILIKO YA TABIA YA NCHI.

Kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi Mkurugenzi huyo anaeleza kuwa kuna mikakati kabambe, imewekwa ya kuanza kutoa elimu na kuhamasisha wananchi namna ya kuvuna na kutunza maji wakati wa msika ili yaweze kutumika wakati wa kiangazi kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji.

“Kuna teknolojia za kisasa ambazo zinatuwezesha kufanya kilimo cha umwagiliaji pale tu ambapo mmea unahitaji maji, pamoja na umwagiliaji wa kutumia matone ili maji machache yanayopatikana yatumike kuzalisha chakula hapa nchini,”anaeleza Kaali.

Baadhi ya Mafanikio katika sekta ya kilimo cha Umwagiliaji katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru.

Kufikia miaka ya 2000 imelezwa kuwa, Serikali imekuwa ikiendelea kuwekeza katika miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji na eneo linalotumika kwa kilimo cha umwagiliaji kwa sasa ni zaidi ya hekta laki sita, (600,000) na kwa kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, inaendelea kupanua eneo la umwagiliaji kufikia hekta 1,200,000 ifikapo mwaka 2025.

Aidha Serikali, imeendelea kuingiza progam mbalimbali katika sekta ya Umwagiliaji kama vile utengenezaji wa mitambo na maboresho ya Miundombinu ya umwagiliaji, kwa kutumia vyanzo vyake vya fedha vya ndani.

Wakulima nchini walikuwa wakilima kwa kutumia njia za asili,Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeendelea kujenga na kuboresha Miundombinu ya kilimo hicho na wakulima wameweza kujiunga katika skimu kupitia vyama vya umwagilia vinavyosajiliwa na Tume ya taifa ya Umwagiliaji hali ambayo inawapa fursa ya wao kulima katika skimu hizo nchini.

Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imetambulisha Ada na Tozo kwa wakulima wa kilimo cha umwagiliaji ili kuendeleza ukarabati wa skimu za umwagiliaji na kuzipatia matunzo, na wakulima wameendelea kupata mafunzo mbalimbali ya kilimo cha umwagiliaji kupitia Technolojia mbalimbali za kisasa zinazotumia maji kidogo,ili kuruhusu maji yaende katika shughuli nyingine za maendeleo na ujenzi wa Taifa,kutoka na mabadiliko ya tabianchi yanayosababisha hali ya ukame na ukosefu wa mvua za uhakika.

Ili kuweza kuhimili na kukabiliana na janga hili,Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imekuwa na mikakati ya kuwa na vyanzo vya uhakika vya maji kama vile teknolojia ya uvunaji wa maji ya mvua kwa kuchimba mabwawa yatakayo tumika katika kilimo cha umwagiliaji wakati wa kipindi cha kiangazi.

Bwana Daudi Kaali, Ameeleza kuwa matumizi ya teknolojia ya sensa yaani vifaa vinavyotumika katika kilimo cha umwagiliaji ambapo mkulima atatumia maji kidogo kwa wakati sahihi, teknolojia ambayo imefanyiwa majaribio katika skimu za kilimo cha umwagiliaji mkoani Iringa, imenufaisha wakulima.

Katika ipindi hiki cha miaka 60 ya Uhuru, Idara ya Usanifu na Utafiti; imeweza kuwa kwenye nafasi kubwa ya kusanifu miradi mbalimbali kwa kutumia wataalam wake wa ndani, tofauti na huko nyuma ambapo Tume ya taifa ya umwagiliaji ilikuwa ikitumia wakandarasi washauri kufanya kazi hizo.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo, Mhandisi Gregory Chigwiye, amesema Idara kwa kutumia wataalam wake wa ndani inaanda na kusanifu miradi kumi, na kuweza kuokoa kiasi cha fedha cha shilingi bilioni moja za kitanzania kama ingetumia mtaalam mshauri kutoka nje.

Mhandisi Chigwiye alisema kuwa, upembuzi yakinifu umekuwa na faida nyingi katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji kwani, kabla ya kuanzisha miradi katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji, upembuzi yanikinifu unasaidia kufahamu kama mradi unaoenda kutekelezwa unatekelezeka na utakuwa na manufaa kwa jamii.

“Tafiti hizi pia zinaweza kusaidia kufahamu kama kunaweza kuwa athari zozote katika mazingira na kuangalia namna ya kuhimili na kukabiliana na hali hiyo.” Alisisitiza.

Mhandisi Naomi Mcharo ni kaimu Mkuu wa Kitengo cha uthibiti Ubora kitengo kinachohusika na uangaliaji wa ubora wa miundombinu inayojengwa pamoja na kazi zinazofanyika katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji.

Mhandisi Mcharo alifafanua kuwa, katika miaka 60 ya uhuru Idara imekuwa na jukumu la kuhakiki na kuangalia ubora ya miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji kuanzia kwenye mipango ya pamoja ya ujenzi.

Kwa Upande wa TEHAMA ,katika kipindi hiki cha miaka 60 ya Uhuu, Serikali imefanya mambo mengi makubwa kama vile kuanzisha taasisi za serikali kama vile Serikali Mtandao EGa, Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA) hizi zote ni Juhudi za Serikali za kuhakikisha kwamba Teknolojia ya habari na Mawasiliano (TEHAMA) inakuwa nyenzo muhimu kwa maendeleo ya mtanzania.

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imenufaika na kuwepo kwa mfumo wa mtandao Serikalini wenye kasi, usalama na uhakika ili kuweza kufanya shughuli za ofisi kiufanisi zaidi.

Serikali pia imefanikisha kuwepo kwa mkongo wa Taifa,kuwepo kwa barua pepe katika Ofisi za umwagiliaji nchi nzima kwa njia salama iliyorahisishwa.

MIRADI KATIKA SEKTA YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI NDANI YA MIAKA 60 YA UHURU

Mhandisi Ntonda Kimasa ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya ujenzi na uendelezwaji wa Miundombinu ya Umwagiliaji Amesema Serikali Kupitia Tume ya Taifa ya umwagiliaji imewekeza katika Miradi Mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji kama ile ya SSIDP, iliyokarabati na kujenga miradi mikubwa ya kitaifa kama DAKAWA na Lower Moshi, miradi ya ASDP, ERPP na TANCAID awamu ya kwanza na ya pili.

Kwa kipindi hiki cha miaka 60 ya Uhuru uzalishaji katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji kwa upande wa mazao ya chakula hususan zao la mpunga umeongezeka kutoa tani 2 kwa heka kwa hadi tani 8 hivisasa.

Pamoja na mafanikio yote haya, Tume ya Taifa ya umwagiliaji ina endelea kujenga miundombinu ya umwagiliaji kwa kutumia wataalam wa ndani ili kuboresha utaalam katika shughuli za ujenzi kama vile wa mabwawa na miundombinu mingine.Hataivyo tume ya Taifa ya Umwagiliaji inawashirikisha wakandarasi wenye zoefu wa kujenga miradi mikubwa ya Umwagiliaji ili kuharakisha Maendeleo ya sekta ya Umwagiliaji.

KILIMO CHA UMWAGILIAJI KWA SASA KINACHANGIA 24% YA CHAKULA NCHINI NA MALENGO KATIKA JAMBO HILI NI KUCHANGIA 50% IFIKAPO MWAKA 2025.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali akizungumza na waandishi wa Habari hawapo pichani, Ofisini kwake jijini Dodoma mapema leo, kuhusu Mafanikio katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji ndani ya kipindi cha miaka sitini ya uhuru.

Post a Comment

0 Comments