Ticker

6/recent/ticker-posts

MISA - TAN YAENDESHA MAFUNZO YA SHERIA KWA WAANDISHI WA HABARI NA CSO's SHINYANGA

Kaimu Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Andrew Marawiti akizungumza wakati akifungua semina kwa waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu sheria mbalimbali zinazosimamia Tasnia ya Habari nchini Tanzania.


************************

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA Tanzania) ikishirikiana na International Media Support (IMS) imeendesha semina kwa waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu sheria mbalimbali zinazosimamia Tasnia ya Habari nchini Tanzania.


Akifungua Semina hiyo leo Jumatatu Desemba 20,2021 Kaimu Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Andrew Marawiti amesema ili waandishi wa habari wafanye kazi katika mazingira mazuri ni vyema wakazijua sheria zilizopo ndiyo maana MISA Tanzania imeendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari.


Marawiti amesema Sheria na Kanuni wanazopaswa kuzielewa vizuri waandishi wa habari ni pamoja na Sheria ya Huduma za Habari -2016, Sheria ya Takwimu - 2019 na Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) 2010.


“Endapo Waandishi wa Habari watazifahamu vyema Sheria na Kanuni zinazosimamia taaluma ya Habari na wataweza kutambua wajibu wao na kutimiza majukumu yao kikamilifu na wataelewa namna ya kukabiliana na changamoto zinazotokana na Sheria hizo”,amesema.


Akiwasilisha mada wakati wa semina hiyo, Mhariri Mwandamizi kutoka Kampuni ya Media Brain Jesse Kwayu amesema ni wajibu wa waandishi wa habari kuzijua sheria zinazohusu tasnia ya habari pamoja na kuzipigia kelele sheria zinazolalamikiwa kukandamiza uhuru wa habari na vyombo vya habari.


Amesema Waandishi wa Habari pamoja na wadau wengine wanapaswa kupaza sauti kuhusu madhaifu yaliyopo katika sheria zinazosimamia tasnia ya habari.


“Ni muhimu Waandishi wa habari wakawa kitu kimoja ili kuwa na nguvu na sauti ya kupaza kuzipigia kelele sheria kandamizi zirekebishwe ili ziwe rafiki kwa walio ndani na nje ya mamlaka za serikali . Tupige kelele ili sheria hizi zirekebishwe, ziwe rafiki kwa kila mtu ndani ya taifa letu”,amesema Kwayu.


“Watu wote wenye nafasi za kurekebisha sheria zinazolalamikiwa kukandamiza uhuru wa habari na vyombo vya habari wafanye kazi ya kuzirekebisha kwa maslahi ya watu wote katika taifa”,ameongeza Kwayu.


Nao washiriki wa semina hiyo wameishukuru MISA Tanzania kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kufanya kazi zao vizuri huku wakiendelea kuandika habari na makala za kushawishi mamlaka zinazohusika ziweze kubadilisha sheria zinazolalamikiwa.


“Sheria hizi ikiwemo sheria ya Takwimu ya mwaka 2019 inaziba mianya kwa waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa sababu bila takwimu kazi ya mwandishi wa habari inakuwa haijakamilika”,amesema Kareny Masasy Mwandishi wa habari Gazeti la Habarileo.


“Tunawashukuru MISA Tanzania kwa mafunzo haya. Sheria na Kanuni zinazoongoza tasnia ya habari ni pana sana tunaomba mafunzo yawe yanatengewa siku nyingi zaidi za mafunzo ili walengwa wanufaike zaidi”,amesema Sam Bahari wa gazeti la Jamhuri.


“Sheria zilizopo zinakanganyana kwa maana kwamba nyingine zinahalalisha na zingine zinaharamisha kitu kimoja kwa hiyo zinabinya uhuru wa mwandishi wa habari katika kutoa taarifa kutokana na kukosa upande wa kufuta. Mafunzo haya yanajenga uelewa kwa waandishi wa habari hivyo kujitambua na kutoa nafasi ya kutekeleza majukumu ya taaluma ya habari”,amesema Jeniva John kutoka Radio Faraja Fm Stereo.


“Haya ni mafunzo mazuri ambayo yanatoa mwanga zaidi kwa waandishi wa habari kuhusu sheria hizi kwani asilimia kubwa kuna mambo mengi ambayo sisi waandishi wa habari tunatakiwa kuishi nazo ili kutoingia katika mgogoro na mamlaka husika. Tuendelee kutoa maoni yetu ili kuboresha sheria hizi kwa maslahi mapana ya taifa la Tanzania”,amesema Isaack Edward kutoka Gold Fm.


“Mafunzo haya yatanisaidia katika utendaji wangu wa kazi pamoja na waandishi wa habari wenzangu kuzifahamu sheria hizi ili kuepuka faini na hatari ya kufungwa jela kwa kukiuka sheria”,amesema Sebastian Mnakaya kutoka Kahama Fm.

“Mafunzo haya yametukumbusha wajibu wetu kwa kufuata sheria zilizopo katika utendaji kazi wetu pamoja na kulinda hadhi ya tasnia ya habari na wanahabari sambamba na kutoingia kwenye matatizo”,amesema Omary Mwambo kutoka Radio Kwizera.


ANGALIA PICHA WAKATI WA SEMINA

Kaimu Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Andrew Marawiti akizungumza wakati akifungua semina kwa waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu sheria mbalimbali zinazosimamia Tasnia ya Habari nchini Tanzania. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Andrew Marawiti akizungumza wakati akifungua semina kwa waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu sheria mbalimbali zinazosimamia Tasnia ya Habari.
Kaimu Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Andrew Marawiti akiwasisitiza waandishi Waandishi wa Habari kuzifahamu sheria mbalimbali zinazosimamia Tasnia ya Habari nchini Tanzania.
Mhariri Mwandamizi kutoka Kampuni ya Media Brain Jesse Kwayu akiwasilisha mada kwenye semina kwa waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga na kupaza sauti kuhusu madhaifu yaliyopo katika sheria zinazosimamia tasnia ya habari ili ziweze kurekebishwa.
Mhariri Mwandamizi kutoka Kampuni ya Media Brain Jesse Kwayu akiwasilisha mada kwenye semina kwa waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga
Waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Mwandishi wa Habari kutoka Radio Faraja Fm Stereo akichangia hoja ukumbini
Waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.

Mwandishi wa habari Sam Bahari akichangia hoja wakati wa semina hiyo
Waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Waandishi Waandishi wa Habari wakiwa ukumbini.
Mwandishi wa habari kutoka Gold Fm, Isaack Edward akichangia hoja ukumbini
Mwandishi wa habari kutoka Radio Kwizera, Omary Mwambo akichangia hoja ukumbini
Mwandishi wa habari wa gazeti la Habarileo Kareny Masasy akichangia hoja ukumbini
Mwandishi wa habari kutoka Kahama FM, Sebastian Mnakaya akichangia hoja ukumbini
Mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru na Mzalendo, Chibura Makorongo akichangia hoja ukumbini
Mwandishi wa habari kutoka Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba akichangia hoja ukumbini
Waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Waandishi Waandishi wa Habari wakiwa ukumbini.
Waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.Waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga wakipiga picha ya pamoja.
Waandishi Waandishi wa Habari na Viongozi wa Asasi za Kiraia (CSO's) mkoa wa Shinyanga wakipiga picha ya pamoja.


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Post a Comment

0 Comments