Ticker

6/recent/ticker-posts

UWT MKOA WA NJOMBE WAKERWA NA KAULI YA MHE.NDUGAI



****************

UMOJA wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT)Mkoa wa Njombe umemtaka Spika wa Bunge wa Spika Job Ndugai kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kuiletea nchi maendeleo badala ya kuwa mpingaji.

Akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari Mwenyekiti wa UWT Mkoa huo Scholastika Kevela alisema kitendo cha Spika huyo kusea nchi inaweza kupigwa mnada kwa kukopa ni kujaribu kutaka kudhohofisha juhudi za kiongozi huyo mkuu wa nchi kuwaletea wananchi maendeleo.


" Hakuna nchi isiyo kopa, pengine hata yeye binafsi ana mikopo..wanaobeza mikopo hawana nia njema na wananchi, wanataka waendelee kubanwa, Rais wetu anakopa mikopo yenye masharti nafuu ili kuutekeleza na kukamilisha miradi yetu mikubwa" alisema Kevela

Alisema kimsingi kauli ya kiongozi huyo mkuu katika Bunge, haina mashiko na zaidi inaonekana ameitoa kwa makusudi kwa sababu anazozijua yeye na pengine watu waliopo nyuma yake, kitu ambacho walisema wao kama UWT hawapo tayari kukifumbia macho.

Kauli ya Mwenyekiti huyo, viongozi mbalimbali wakiwemo waaandamizi na waliowahi kuwa wabunge pamoja na wanaharakati mbalimbali na baadhi ya wanachama wa vyama pinzani, imekuja kufuatia kauli iliyotolewa na Spika Ndugai kuwa kitendo cha nchi kukopa ni kutaifanya ipigwe mnada.

" Kama ameitoa akiwa na nia kutaka kumvunja moyo ili asigombee mwaka 2025, atambue kuwa sisi Wanawake na watanzania wengi tulishasema kuwa Rais Samia mitano tena, aachwe afanye kazi yake kutuletea maendeleo" alisisitiza Mwenyekiti huyo



Alisema tangu aingie madarakani zaidi ya miezi tisa iliyopita, Rais Samia Suluhu Hassan amelifanyoa Taifa mambo mengi na makubwa kiasi cha kufanya uongozi wake uumvitie kila mtu yakiwemo mataifa mbalimbali.




Alisema wao kama wanachama wa chama hicho watahakikisha kuwa wakati wote wanasimama imara na kumtetea Mwenyekiti wao wa chama Taifa kwa kuwa ameonyesha dhamira ya kweli kutatua changamoto za wananchi.

Post a Comment

0 Comments