Ticker

6/recent/ticker-posts

WAJASIRIAMALI WA UKANDA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKA WAPONGEZWA KWA UBUNIFU

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Shaaban akizungumza na wajasiriamali na wakazi wa Mwanza alipotembelea Maonesho ya 21 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Afrika Mashariki maarufu kama Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika katika Viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza, Desemba 12, 2021.Sehemu ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Shaaban (hayupo pichani).


Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilagi akieleza jambo wakati wa hafla ya kufunga maonesho ya 21 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Afrika Mashariki maarufu kama Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika katika Viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza, Desemba 12, 2021.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Shaaban akiwa ameambatana na viongozi na waratibu alipotembelea mabanda ya wajasiriamali katika maonesho ya 21 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Afrika Mashariki maarufu kama Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika katika Viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza, Desemba 12, 2021.

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Shaaban akiangalia bidhaa za Sanaa alipotembelea banda la wajasiriamali kutoka Rwanda katika maonesho hayo.


Mkurugenzi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi Bw. Ally Msaki (kulia) akieleza jambo kwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Shaaban (wa pili kutoka kushoto). Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Jamal Katundu. Wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilagi.


Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Shaaban akiangalia bidhaa inayotengenezwa na mjasiriamali bora kutoka Kenya Bw. Geoffrey Njuguna (kulia). Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara na Forodha wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Kenneth Bagamuhunda.

PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

************************

Na: Mwandishi Wetu – Mwanza

Wajasiriamali kutoka nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wapongezwa kwa ubunifu wa kutengeneza bidhaa zinazotokana na malighafi zinazopatikana katika ukanda huo.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Shaaban alipotembelea Maonesho hayo ya 21 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Afrika Mashariki maarufu kama Nguvu Kazi au Jua Kali hii leo Desemba 12, 2021 katika Viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza.

Waziri huyo alieleza kuwa, kupitia maonosho hayo ya Nguvu Kazi au Jua Kali ambayo yanalenga wajasiriamali wadogo na wa kati katika sekta isiyo rasmi yamekuwa ni chachu ya mafanikio ya wajasiriamali kuwafanya wawe wabunifu na kuwapatia fursa mbalimbali ya kujifunza kutoka kwa wenzao wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Nimetembelea mabanda ya wajasiriamali wa nchi mbalimbali na nimeshuhudia ubora wa bidhaa zao zikiwa na utofauti mkubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma na muonekano wa bidhaa zao nilizoziona hapa leo hakika kuna mabadiliko makubwa sana, endeleeni na juhudi Zaidi kutumia fursa zinazopatikana katika nchi zetu za Jumuiya ya Afrika Mashariki,” alisema Waziri Shaaban

“Kutokana na ubora wa bidhaa zenu ni hakika kuwa sasa mnauwezo wa kuuza kwa wingi bidhaa kwa wingi ndani ya nchi na hata nje ya nchi zetu za Jumuiya ya Afrika Mashariki,” alieleza

Aliongeza kuwa, katika maonesho hayo wajasiriamali wameweza kupata fursa ya kushiriki kwenye makongamano ambapo mada mbalimbali zimejadiliwa ikiwa ni pamoja na biashara za mipakani (Cross Border Trade and Non – Trade Tariff Business), fursa za uwekezaji katika miongoni mwa nchi wanachama na kutoa elimu ya ufanyaji wa biashara kwa zao na nchi wanachama kwa ufanisi.

Sambamba na hayo Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Shaaban alisema kuwa Serikali za nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinaendelea kushughulikia chanagamoto zinazowakabili wajasiriamali ili kuzipatia ufumbuzi utakao wawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi na kuleta tija.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilagi alisema kuwa maonesho hayo yametoa fursa kwa wakazi wa Mwanza na wananchi kutoka maeneo ya jirani kununua bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wa ukanda wa Afrika Mashariki. Pia alisema kuwa wajasiriamali wamepata fursa ya kukuza teknolojia ya utengezaji wa bidhaa zao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Biashara na Forodha wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Kenneth Bagamuhunda alieleza kuwa maonesho hayo ya 21 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Afrika Mashariki maarufu kama Nguvu Kazi au Jua Kali yamekuwa na mvuto kutokana na asilimia 80 ya wajasiriamali walioshiriki ni wanawake na zaidi ya asilimia 60 ni vijana.

Awali Mwenyekiti wa Shirikisho la Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ameishukuru Serikali kwa kuridhia na kufadhili maonesho hayo ambayo yamewasaidia wajasiriamali wengi nchini kujifunza utengenezaji wa bidhaa bora, kuimarisha ushirikiano na kukuza masoko ya bidhaa zao.

Post a Comment

0 Comments