Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MKUU MAJALIWA, SPIKA NDUGAI WAONGOZA MAPOKEZI YA TIMU YA BUNGE SPORTS CLUB IKIJIZOLEA JUMLA YA VIKOMBE 7 KATIKA MICHEZO YA EALA


Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai wakiwa tayari kuwapokea wachezaji wa timu ya Bunge Sports Club watakapowasili katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, Disemba 18, 2021, wakitokea Jijini Arusha katika michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akimpongeza kwa namna yake mchezaji wa mchezo wa kuvuta kamba wa timu ya Bunge Sports Club, Mhe. Mussa Sima wakati timu hiyo ilipowasili katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, Disemba 18, 202, kutoka kwenye michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha


Wachezaji wa timu ya Bunge Sports Club wakimsikiliza Spika Ndugai akizungumza baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge wakitokea Jijini Arusha katika michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Disemba 18, 2021

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akipokea kombe la mchezo wa mpira wa miguu kutoka kwa nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya Bunge Sports Club, Mhe. Cosato Chumi wakati walipowasili kutoka Jijini Arusha kwenye michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Disemba 18, 2021, kulia ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akimkabidhi Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kombe la mpira wa miguu ikiwa ni moja ya kati ya vikombe saba walivyopata baada ya kuibuka washindi katika michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyofanyika Jijini Arusha, Disemba 18, 2021


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na wachezaji wa timu ya Bunge Sports Club na watumishi wa ofisi ya Bunge wakati walipowasili kutoka Jijini Arusha kwenye michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Disemba 18, 2021


Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wachezaji wa timu ya Bunge Sports Club na watumishi wa ofisi ya Bunge wakati walipowasili kutoka Jijini Arusha kwenye michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Disemba 18, 2021

Post a Comment

0 Comments