Ticker

6/recent/ticker-posts

HADI KUFIKIA JUNI, 2022 JUMLA YA WATU 706,396 WATAKUWA WAMECHANJA MKOANI IRINGA


****************************

Na. WAMJW - IRINGA

Watu 706,094 wanataraijiwa kuwa wamechanja chanjo dhidi ya UVIKO-19 Mkoani Iringa hadi kufikia mwezi June mwaka huu, ambapo hadi sasa watu waliopata huduma ya chanjo ni 29,094.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Queen Sendiga alipokuwa anaongea na waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa na Njombe katika mafunzo yaliyoandaliwa na Wizara ya afya kupitia Mpango wa Taifa wa chanjo.

"Katika mpango shirikishi na harakishi wa uchanjaji chanjo ya UVIKO-19, Mkoa wa Iringa tunategemea kutekeleza shughuli kama uchanjaji kwa njia ya Mkoba, kuelimisha jamii kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo kwa wanahabari na njia za magari." Amesema Mhe. Sendiga

Sendiga amesema baada ya mapokezi hayo Mkoa wa Iringa umeweza kuchanja jumla ya watu 17,314 dozi ya kwanza ya Sinopharm sawa na watu 17,314 na dozi ya pili watu 8,007 na dozi ya kwanza ya Pfizer ni watu 9,298 na ya pili watu 606.

Aidha, Mkuu wa mkoa huyo amewashauri wananchi waliopata dozi ya kwanza baada ya siku 21 kufika katika vituo vya kutolea huduma kupata dozi ya pili ili kuendelea kuweka kinga ya mwili.

"Kwa wale ambao bado hawajapata chanjo wakapate chanjo ili kuweka kinga mwilini hii inasaidia virusi vikiingia mwilini vikapambane na kinga ya mwili iliyowekwa." amesema Mhe. Sendiga

Kwa upande wake Afisa programu mpango wa Taifa wa chanjo wizara ya Afya Bi.Lotalis Gadau amewatoa hofu watanzania kuwa chanjo ni salama na haina madhara kwa anaechanja.

"Mimi nimechanja mwezi wa Saba Mwaka Jana lakini nipo vizuri hadi sasa sijapata madhara yoyote na nina mifano mingi ya watu waliochanja hawakupata madhara." amesema Gadau

Mkoa wa Iringa unaunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan juu ya mapambano ya ugonjwa wa Corona kwa kuendelea kuhamasisha chanjo zote za watoto na wakubwa na hasa chanjo ya UVIKO-19.

Mkoa wa Iringa kuanzia mwezi Oktoba,2021 hadi Januari 8,2022 umepokea jumla ya dozi 29,250 za chanjo ya Pfizer na dozi 51,832 za chanjo ya Sinopharm kutoka Wizara ya Afya.

Baada ya Mafunzo hayo kwa waandishi wa Habari baadhi ya washiriki walipata chanjo ya UVIKO-19 iliyoongozwa na mtoa huduma Oda Mwinuka.

Post a Comment

0 Comments