Ticker

6/recent/ticker-posts

HII HAPA IDADI YA MAKADA WA CCM WALIOJITOSA USPIKA,HAIJAWAHI KUTOKEA VIGOGO WAFURIKA


Katibu msaidizi mkuu Idara ya Oganazesheni CCM Solomon Itunda, akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 15,2022 jijini Dodoma wakati akitangaza kufungwa kwa zoezi la uchukuaji fomu kwa ajili ya kugombea Uspika katika siku ya mwisho wa zoezi hilo ambapo wanachama wa CCM wamefika 71.

.................................................

Na.Alex Sonna,Dodoma

JUMLA ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) 71 wamechukua fomu za kuomba ridhaa ya kugombea Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kujaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya Job Ndugai kujihuzulu hivi karibuni.

Katibu msaidizi mkuu Idara ya Oganazesheni CCM Solomon Itunda, akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 15,2022 jijini Dodoma amesema kuwa idadi ya wanachama waliochukua fomu katika siku ya mwisho wa zoezi hilo imefika 71.

Bw.Itunda amesema kuwa kwa siku ya jana jumla ya wanachama watano walichukua fomu na kufanya idadi kufikia wanachama 71 baada ya wale 66, waliokuwa wamechukua hadi juzi.

“Leo hii tumepokea wanachama watano ambao wamejitokeza katika vituo vyetu vya Dodoma na Dar es saalam kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi hii ya Uspika iliyoachwa wazi.

Aidha, amesema katika kituo cha Dodoma mwanachama mmoja ndiye aliyejitokeza kuchukua fomu wakati katika ofisi ya Lumumba ni wanachama wanne na afisi kuu ya Zanzibari hakuma aliyechukua

Itunda,amemtaja aliyechukua fomu ofisi kuu Dodoma kuwa ni Samwel Magero.

“Ofisi ndogo ya Lumumba waliochukua fomu ni Rahimuddin Ismail, Alex Mwita,Themistocles Laurian Rwegasira pamoja na Grangay Nyalohala”amesema

Amesema kuwa kukamilika kwa zoezi hilo la kuchukua fomu lililoanza Januari 10 mwaka huu kunatoa nafasi kwa vikao vingine kuanza.

“Baada ya zoezi hili la kuchua na kurejesha fomu sasa hatua inayofuata ni vikao vingine kuketi ili kuanza kufanya mchujo wa kupitisha jina moja litakalo kiwakilisha chama katika kugombania nafasi hii ya Uspika”ameeleza

Post a Comment

0 Comments