Ticker

6/recent/ticker-posts

MATUKIO KATIKA PICHA: NAIBU WAZIRI UMMY AKIKABIDHI CHEREANI SITA KWA KIKUNDI CHA WENYE ULEMAVU CHAMANANGWE PEMBA


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kojani na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Hamad Chande wakikabidhi chereani kwa mwakilishi wa kikundi cha watu wenye ulemavu Bi. Asha Issa Kombo (wa kwanza kushoto) wanaojifunza ushonaji wa nguo katika eneo la Chamanangwe Wilaya ya Wete Pemba. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Bw. Ussi Debe na wa pili kutoka kushoto ni Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Mhe. Amhed Aboubakar Mohamed.


Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu(Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza na wanakikundi wa Chamanangwe (wenye ulemavu) wanaojifunza ushonaji wa nguo, alipowatembelea na kukabidhi chereani sita katika eneo la hilo katika Wilaya ya Wete visiwani Pemba Januari 4, 2022.


Mbunge wa Jimbo la Kojani na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Hamad Chande akizungumza wakati hafla ya kukabidhi chereani sita katika eneo la Chamanangwe katika Wilaya ya Wete visiwani Pemba Januari 4, 2022.


Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu(Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kojani na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Hamad Chande wakiangalia nguo zilizoshonwa na wanakikundi wenye ulemavu waliopo Chamanangwe katika Wilaya ya Wete visiwani Pemba, mara baada ya kuwakabidhi chereani sita zilizotolewa na mbunge huyo kwa kushirikiana na Serikali.


Fundi wa ushonaji Bi. Aziza Kombo akichukua vipimo vya nguo vya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga mara baada ya kugawa chereani kwa kikundi cha watu wenye ulemavu wanaojishughulisha na ushonaji Pemba.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga akifurahi pamoja na Bi. Asha Issa Kombo anayejifunza ushonaji nguo mara baada ya zoezi la kukabidhi chereani sita kwa lengo la kuunga mkono jitihada za watu wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi Chamanangwe Pemba wakati wa ziara yake ya kikazi.


Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu(Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga pamoja na ugeni alioongozana nao wakiwa katika picha ya pamoja na wanakikuchi hao, mara baada ya zoezi la kukabidhi chereani hizo zinazolenga kuwawezesha katika shughuli za kujikwamua kiuchumi Chamanangwe katika Wilaya ya Wete visiwani Pemba

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Post a Comment

0 Comments