Ticker

6/recent/ticker-posts

MBEYA :WATATU MBARONI KWA TUHUMA ZA WIZI WA PIKIPIKI


...............................................

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa watatu 1. BILIER PATRICK [32] 2. MESHACK MGALA [25] na 3. IBRAHIM MGALA [22] wote wakazi wa itumbi wilayani Chunya kwa kosa la kupatikana na mali za wizi Pikipiki.

Watuhumiwa kwa Pamoja walikamatwa mnamo tarehe 13.01.2022 majira ya saa 10:00 asubuhi huko Kijiji cha Itumbi, Kata ya Matundasi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya katika Misako dhidi ya watuhumiwa wa wizi wa Pikipiki na makosa mengine.

Watuhumiwa baada ya kuhojiwa na kupekuliwa walikutwa na Pikipiki yenye namba za usajili MC.169 CER aina Blast, Guta Na.MC 782 CWD aina ya Sinoray na injini ya guta Na. ZDCG-AS767M0310AG-GZ13 ambavyo vyote ni mali za wizi. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

KUKAMATWA KWA WAHAMIAJI HARAMU.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtanzania mmoja dereva wa lori la mafuta mali ya kampuni ya UKOD OIL aliyefahamika kwa jina la BROWN LARISA [46] Mkazi wa Dar-es-Salaam aliyekuwa akiendesha Gari yenye namba za usajili T. 983 BNT na tela Na.T. 902 DFS aina ya Benz kwa kosa la kusafirisha wahamiaji haramu raia wa nchini Ethiopia.

Mtuhumiwa na wahamiaji hao walikamatwa mnamo tarehe 13.01.2022 majira ya saa 21:00 usiku huko Mabadaga, Kata ya Mapogoro, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya akitokea Dar es Salaam kuelekea nchini Malawi.

Wahamiaji haramu waliokamatwa wametambulika kwa majina ya 1. MARLESA YAKOB [18] 2. DAGAFA PETRO [26] 3. SAMWEL MALAKU [18] na 4. Abi MITIKU [26] wote rai ana wakazi wa nchini Ethiopia.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA WIZI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili 1. OWEN USWEGE MWAMBELA [21] na 2. ROBERTY PAUL FUMBO [22] wote wakazi wa Njisi wilayani Kyela kwa tuhuma za kupatikana na mali mbalimbali za wizi.

Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 13.01.2022 majira ya saa 19:00 usiku huko Kitongoji na Kata ya Njisi, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya katika msako ulioendeshwa na Jeshi la Polisi dhidi ya wahalifu wa matukio mbalimbali.

Katika msako huu, watuhumiwa walikutwa na mali za wizi nguo aina mbalimbali zikiwemo Tshirt 29, Suruali 22, Kaptula 22, Bukta 18, nguo za ndani 06, Pazia 02, Gauni 01 na mikanda ya suruali 06 vyote vikiwa thamani ya Tshs 1,500,000/= ambavyo ziliibwa tarehe 13.01.2022 majira ya saa 05:00hrs huko eneo la Stendi ya zamani vikiwa safarini kutoka Tanzania kupelekwa Malawi mali ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la SAJENT ANYITIKE MWAISELO [35] Mkazi wa Kijiji cha Ibanda.

Imetolewa na:

[CHRISTINA A. MUSYANI – ACP]

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Post a Comment

0 Comments