Ticker

6/recent/ticker-posts

MSEMAJI MPYA WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI AFANYA ZIARA MAGEREZA.


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini Meja Jenerali Suleiman Mzee (mwenye suti ya bluu) akizungumza na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ndiye Msemaji wa Jeshi hilo Kamishna Msaidizi Mwandamizi, SACF Puyo Nzalayaimisi (wa pili kushoto) alipotembelea Ofisi za Makao Makuu ya Magereza Msalato Dodoma kwa lengo la kujitambulisha, leo tarehe 24 Januari, 2022.


Mkuu wa Kitengo cha Habari, Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ndiye Msemaji wa Jeshi hilo Kamishna Msaidizi Mwandamizi, SACF Puyo Nzalayaimisi (kulia) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuingia katika ofisi ya Msemaji wa Jeshi la Magereza nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Justine Kaziulaya, ndc (kushoto) alipofanya ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Magereza kujitambulisha leo tarehe 24 Januari, 2022.


Msemaji wa Jeshi la Magereza nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Justine Kaziulaya, ndc (kushoto) akimsindikiza Mkuu wa Kitengo cha Habari, Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ndiye Msemaji wa Jeshi hilo Kamishna Msaidizi Mwandamizi, SACF Puyo Nzalayaimisi (katikati) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Makao Makuu ya Magereza Msalato Dodoma, leo tarehe 24 Januari, 2022.

**************************

Msemaji Mpya na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) Puyo Nzalayaimisi leo tarehe 24 Januari 2022 amefanya ziara ya kujitambulisha Jeshi la Magereza alipomtembelea Msemaji wa Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Justine Kaziulaya, ndc katika ofisi za Makao Makuu ya Magereza Msalato Dodoma. SACF Nzalayaimisi alipokelewa na mwenyeji wake SACP Kaziulaya na baadae kukutana na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini (CGP) Meja Jenerali Suleiman Mzee kwa ajili ya kujitambulisha.

Kamishna Jenerali Mzee ambaye amefurahishwa sana na ugeni, amesema Ushirikiano baina ya Majeshi yetu ni kitu kizuri kwani kinatuweka karibu na kutuongezea Morali katika utendaji wetu wa kazi pia ametutaka kutokubweteka na kutaka tuwe wabunifu kwa maslahi mapana ya Jeshi na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Msemaji Mpya na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji SACF Puyo Nzalayaimisi, ameshukuru kwa mapokezi mazuri na kuahidi kuyafanyia kazi yale yote yaliyozungumzwa.

Naye Msemaji wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Justine Kaziulaya, ndc amemuahidi ushirikiano zaidi SACF Nzalayaimisi katika masuala mbalimbali ya kihabari kwa manufaa ya majeshi yenyewe, Wizara na Taifa kwa ujumla.

(Picha zote na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)

Post a Comment

0 Comments