Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DKT.HUSSEIN ALI MWINYI AMTUNUKU NISHANI YA MAPINDUZI RAIS MSTAAFU MHE.DK.ALI SHEIN


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimvisha Nishani ya Mapinduzi Rais wa Zanzibar Mstaafu wa Awamu ya Saba Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 11-1-2022.(Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa amesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa wa Zanzibar, Tanzania na wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika hafla ya kutunuku Nishani ya Mapinduzi kwa Rais wa Zanzibar Mstaafu wa Awamu ya Saba Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein,iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS Mstaafu wa Zanzibar wa Awamu ya Saba Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akiwa amesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa wa Zanzibar,Tanzania na wa Afrika Mashariki katika hafla ya kutunuku kwa Nishani ya Mapinduzi na (kushoto kwake) Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu Balozi Seif Ali Iddi na Kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Khamis Ramadha Abdalla.(Picha na Ikulu)  

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Saba Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, baada ya kumtunuku Nishani ya Mapinduzi, hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 11-1-2022.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments