******************
NA EMMANUEL MBATILO
Leo mechi mechi mbili zimechezwa katika michuano ya Mapinduzi Cup ambapo Simba Sc iliingia uwanjani jioni ya leo kuvaana na timu ya Selem View na kufanikiwa kuondoka na Ushindi wa mabao 2-0.
Mabao ya Simba Sc yaliwekwa kimyani na nyota wao Pape Sakho akiifunga dakika ya 25 ya mchezo kipindi cha kwanza, na bao la pili likifungwa na kiungo wao Bwalya dakika ya 53 ya mchezo.
Katika mechi nyingine iliyopigwa usiku huu ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo Yanga wakimenyana na timu ya Taifa ya Jang'ombe na kufanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-0.
Mabao ya Yanga yalifungwa na na mshambuliaji wao Ebenezer Makambo pamoja na nyota mpya waliomsajili hivi karibuni Denis Nkane.
0 Comments