Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MULAMULA AWAHIMIZA MABALOZI KUTEKELEZA DIPLOMASIA YA UCHUMI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb.) amewasisisita mabalozi wa Tanzania wanaowakilisha nje ya nchi kuweka mpango kazi wa utekelezaji wa majukumu ya kidiplomasia wenye maslahi mapana kwa uchumi wa Taifa.

Mhe. Mulamula ameyasema hayo alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Mhe. Said Shaibu Mussa aliyekuja kumuaga ofisisni kwake leo tarehe 14 Januari 2022 katika ofisi za Wizara, jijini Dodoma.

Mazungumzo baina ya wawili hao yalijikita katika kuangalia namna bora ya kuboresha utendaji wa ofisi za balozi za Tanzania sambamba na Wizara ili kuweza kutumia fursa zilipo kunufaisha Taifa.

“Nasisistiza balozi zetu kutekeleza majukumu kwa kuhakikisha fursa za kiuchumi zinawekewa msisistizo sambamba na mafanikio yanayopatikana yanatangazwa kikamilifu ili kuweza kuuhabarisha uuma namna ya kuzitumia fursa zinazopatikana”. Alisema Mhe. Waziri

Pia ameeleza umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja ili kuweza kufikia malengo tarajiwa katika sekta ambazo serikali ya Tanzania imeingia makubaliano ya ushirikiano na mataifa wanayowakilisha.

Naye Balozi Said Shaibu Mussa amemshukuru Mhe. Waziri kwa maelekezo ya kiteundaji aliyoyapata sambamba na kuahidi kufanya kazi kwa ubunifu katika majukumu hayo mapya ili kuongeza maeneo ya ushirikiano baina ya Tanzania na Kutwait.

Tanzania na Kuwaita zimekuwa zikishirikiana katika sekta za kilimo, afya, ujenzi wa miundombinu ya barabara na Maji.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (kulia) amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Mhe. Said Shaibu Mussa alipokuja kumuaga ofisini kwake leo tarehe 14 Januari 2022 jijini Dodoma.
Mazungumzo yakiendelea. Kulia ni Msaidizi wa Waziri, Bw. Seif Kamtunda akifatilia mazungumzo.
Mhe. Waziri Mulamula akimkabidhi vitendea kazi Mhe. Said Mussa.

Post a Comment

0 Comments