Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI UMMY: TUTAWAPIMA WATOA HUDUMA ZA AFYA NCHINI KWA MAMBO SITA


Waziri wa afya Ummy Mwalimu na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Kituo cha Afya Makorora leo kushoto mwenye koti ni Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makorora Neema Charles

Waziri wa afya Ummy Mwalimu na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) kushoto akikisistiza jambo kwa Mfamasia wa Kituo cha Afya Makorora Glory Urio wakati wa ziara yake kwenye kituo hicho

Waziri wa afya Ummy Mwalimu na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) kushoto akikagua dawa kwenye Kituo cha Afya Makorora wakati wa ziara yake



WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amesema watawapima watoa huduma za afya nchini kwa kuangalia maeneo makubwa sita katika hospitali za serikali ikiwemo mapokei ambayo mgonjwa anapewa pamoja na lugha kutoka kwa watumishi.

Ummy aliyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kutembelea kituo cha Afya Makorora Jijini Tanga ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea eneo la kuhifadhiwa dawa kwenye kituo hicho ambapo atawapima watoa huduma zao kuanzia Hospitali za Taifa, Rufaa,Mikoa,wilaya,Zahanati na Vituo vya Afya.

“Lakini lazima tuangalie je mgonjwa anatakiwa kupata kipimo cha Utra Soud,Malaria,UTI na Je amepata vipimo vyote ndani ya kituo …wataangalia je mgonjwa amepewa dawa anazostahili ndani ya kituo husika na sio kuambiwa akanunue nje “Alisisitiza.

Akiwa katika kituo amebaini kuwepo kwa changamoto bohari ya dawa wana mpango mzuri wa kutoa hudunma kwa ajili ya watoto wachanga vinavyozaliwa na upungufu,wameoda vifaa kutonma MSD toka mwaka jana Octoba mwaka 2021 mpaka leo MSD wameshindwa kusema vifaa wanavyo au la.

Wameorder vifaa MSD toka mwaka jana 2021 na vifaa vyenyewe siyo vingi cha kushangaza mpaka leo MSD ameshindwa kusema vifaa kama anavyo au hakuna hii ndio maana juzi katika, maelezo yangu nilisema tutaangalia mnyororo mzima wa dawa katika ununuzi, usambazaji na usafirishaji wa dawa kuanzia ngazi ya kituo mpaka MSD, "amebainisha Waziri Ummy.

Waziri Ummy alisema pia mambo mengine ni muda ambao mgonjwa aliotumia kupata huduma ikiwemo ameingia wakati gani na kupata vipimo kwani vipaumbele vya awali ya sita ni kuwekeza kwenye ubora wa huduma.

Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora za afya na si bora tu huduma kwa kuangalia maeneo hayo 6.


"Kipaumbele cha awamu ya sita kitakuwa ni kuwekeza kwenye huduma bora za afya tunataka kutofautisha hospitali na waganga wa kienyeji ikumbukwe mganga wa kienyeji yeye hapimi afya lakini hospitali ni tiba na huduma za kiuchunguzi kitaalamu, " Aliisitiza Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema baada ya kutembelea kituo cha Makorora wamebaini mambo mawili ikiwemo changamoto ya bohari ya dawa licha ya wao kuwa na mpango mzuri wa kutoa huduma kwajili ya watoto wachanga wanaozaliwa na uzito pungufu.

Wakati huo huo Waziri Ummy amepiga marufuku hospitali zote nchi nzima kuacha kuwatoza fedha kina mama wajawazito nchi nzima na badala yake huduma zote zinazopatikana wapatiwe bure ikiwa ni pamojana huduma ya Ultra sound pamoja na watoto wachanga zitolewe bure ili kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga.


"Mnapoweka kikwazo cha elfu 40 kwa jili ya vipimo kina mama wengi tutawakosa nyie wenyewe mnajua hudhurio la kwanza la mama mjamzito kliniki ni chini ya asilimia 50 wajawazito wengi wanashindwa kuja kliniki mapema kwasababu ya michango na matizo yasiyokuwa namaana tunayawatoza hii ni sera ya afya hatujaifuta na hatujaibadilisha, "amesisitiza Waziri Ummy.

Post a Comment

0 Comments