Ticker

6/recent/ticker-posts

YANGA SC KUMILIKI KADI ZA KIDIGITALI KWA WANANCHAMA WAKE

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Fredrick Mwakalebela(kulia) na mtendaji mkuu wa klabu ya Yanga Senzo Mazingiza wakisaini mkataba wa makubaliano na Kampuni za KILINET na N-Cards kwa ajili ya kutengeneza kadi za kidigitali zitazokuwa zinatumiwa na Wanachama wa klabu hiyo ikiwa ni sehemu ya hatua za awali kwenye mfumo mpya wa uendeshaji, kadi
moja itauzwa TZS 29,000.
Mkurugenzi mtendaji wa Kilinet Mohammed Saleh akisaini mkataba wa makubaliano na Klabu ya Yanga kwa ajili ya kutengeneza kadi za kidigitali zitazokuwa zinatumiwa na Wanachama wa klabu hiyo ikiwa ni sehemu ya hatua za awali kwenye mfumo mpya wa uendeshaji, kadi
moja itauzwa TZS 29,000
Mkuu wa bidhaa ya N-Card Khalifa Mwinyi akisaini mkataba wa makubaliano na klabu ya Yanga kwa ajili ya kutengeneza kadi za kidigitali zitazokuwa zinatumiwa na Wanachama wa klabu hiyo ikiwa ni sehemu ya hatua za awali kwenye mfumo mpya wa uendeshaji, kadi moja itauzwa TZS 29,000

**************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Klabu ya Young Africans Sports Club wamesaini mkataba wa makubaliano na Kampuni za KILINET na N-Cards kwa ajili ya kutengeneza kadi za kidigitali zitazokuwa zinatumiwa na Wanachama wa klabu hiyo ikiwa ni sehemu ya hatua za awali kwenye mfumo mpya wa uendeshaji, kadi moja itauzwa TZS 29,000.


Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa bidhaa ya N-Card Khalifa Mwinyi amesema mara baada ya kuingia mkataba huo na Klabu ya Yanga, Mashabiki wa Yanga wataweza kutumia kadi zao aidha ya kadi ya Mwanachama au ya Mshabiki ataweza kutumia kadi hiyo kununua tiketi yake kidigitali na kuweza kuingia uwanjani moja kwa moja, lakini pia kadi hiyo ataweza kulipia malipo mbalimbali.

"N-Card tunashukuru sana kuaminiwa na Klabu ya Yanga kuwa moja ya wadau ambao tutashiriki katika mchakato wa kihistoria wa kuleta mageuzi katika Klabu ya Yanga na maendeleo ya soka kwa Ujumla". Amesema Mwinyi.

Nae Mkurugenzi mtendaji Kilinet Mohammed Saleh amesema Jukumu la Kilinet ni kuangalia na kuzifanyia kazi michakato na mikakati ya Yanga kwa kutumia teknolojia za kisasa.

"Leo imekuwa siku ya kihistoria na sasa hivi klabu ya Yanga inaenda katika mabadiliko ya kidigitali na Kilinet tumepata fursa ya kufanya kazi na Yanga kuleta teknolojia za kisasa kwa ajili ya kuliwezesha ili jambo kufanyika kikamilifu". Amesema Saleh.
Post a Comment

0 Comments