Ticker

6/recent/ticker-posts

ZUHURA YUNUS KUACHANA NA BBC BAADA YA MIAKA 14


**********

Mtangazaji mashuhuri wa BBC Zuhura Yunus anaondoka katika shirika hilo baada ya kulitumikia kwa takriban miaka 14 .

Zuhura atatangaza kipindi chake cha mwisho cha Dira ya Dunia mwendo saa tatu usiku saa za Afrika mashariki. Hata hivyo amebakiza siku kadhaa za likizo kabla ya kuondoka rasmi.

Mtangazaji huyo aliyejiunga na BBC Swahili mwaka wa 2008 amesema anataka kuutumia muda wake sasa kuendelea na uandishi na mambo mengine nje ya BBC.

Taarifa ya Zuhura kuondoka BBC inakuja miezi kadhaa baada ya kuandika kitabu chake cha wasifu wa Biubwa Amour Zahor mwanaharakati mwanamke wa kisiasa wakati wa mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.

Post a Comment

0 Comments