Ticker

6/recent/ticker-posts

DELLAH CAR TRADERS YATIMIZA MIAKA MITATU, YAFUNGUA OFISI MPYA SHINYANGA MJINI


Paroko wa Parokia ya Ngokolo Jimbo Katoliki Shinyanga, Padre Adolf Makandago (kulia) na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge wakikata utepe kufungua rasmi ofisi Mpya za Kampuni ya Dellah Car Traders zilizopo katika Ghorofa ya Pili katika Jengo la NSSF Mjini Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kampuni ya Uagizaji wa Magari aina zote nje ya nchi maarufu Dellah Car Traders Company imefungua rasmi Ofisi Mpya katika jengo la NSSF Mjini Shinyanga ikiwa ni sehemu ya sherehe ya kutimiza miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Kampuni hiyo pamoja na sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company,Edwin Charles Dellah.

Sherehe hizo ambazo pia zimehudhuriwa na watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima ‘Shinyanga Society Orphanage Centre’ kilichopo Bushushu kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga zimefanyika leo Jumapili Februari 28,2022 katika ukumbi wa NSSF Mjini Shinyanga mahali ambapo Kampuni ya Dellah Car Traders Company imefungua ofisi mpya.

Akizungumza wakati wa sherehe hizo,Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company, Edwin Charles Dellah amesema Februari 27 ndiyo siku aliyozaliwa lakini pia ni tarehe ambayo ndiyo alianzisha Kampuni ya uagizaji magari kutoka Japan, Dubai, Singapore na UK hivyo ameona ni vyema watumie tarehe hii kufungua rasmi ofisi yao mpya katika jengo la NSSF Mjini Shinyanga.

“Awali ofisi yetu ilikuwa katika jengo la Seif barabara ya kwenda Stendi ya Zamani Mjini Shinyanga na sasa tumehamia ghorofa ya Pili katika jengo la NSSF Mjini Shinyanga mkabala na barabara ya Shinyanga – Mwanza. Ofisi zetu zingine zipo Jijini Dar es salaam pale Magomeni Usalama. 3D Building, 2nd Floor,Adjacent Watumishi Housing”,amesema Dellah.

“Huduma tunazotoa ni pamoja na ushauri wa magari kulingana na matumizi,tunakufikishia gari ndani nan je ya Tanzania. Pia tunatoa ushauri wa kodi za magari,tunatoa taarifa za mara kwa mara pindi unapoagiza gari nasi na tunakutafutia gari uipendayo na kukuagizia kwa gharama nafuu sana. Hali kadhalika tunatoa ofa ya Fire Extinguisher na Triangle Reflector, usajili wa gari bure na plate number pamoja na bima bure mwaka mmoja”,ameeleza Dellah.

Katika hatua nyingine Dellah amesema ameamua kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ‘Birthday’ kwa kukata keki na kula chakula cha pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kuonesha upendo kwa watoto hao lakini pia kusherekea miaka mitatu na kuzindua ofisi mpya kwa kualika wadau mbalimbali wa Kampuni ya Dellah Car Traders.

Aidha amewapongeza wadau wote walioshiriki katika sherehe hizo huku akiwaomba wadau kuendelea kuiamini Kampuni ya Dellah Car Traders kwa kuagiza magari aina zote kutoka Japan, UK, Dubai na Singapore.

“Karibuni sana Dellah Car Traders Company. Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba +255 763 370 454 au +255 756 330 333 au +255 746 550 551. Email : sales@dellahcartraders.co.tz , Instagram : dellah_car_traders_ltd ,Website : www.dellahcartraders.co.tz",ameeleza Dellah.


Akizungumza baada ya kuweka Wakfu ofisi za Kampuni ya Dellah Car Traders Company, Paroko wa Parokia ya Ngokolo Jimbo Katoliki Shinyanga, Padre Adolf Makandago amempongeza Mkurugenzi wa Kampuni hiyo kwa kuanzisha huduma ya uagizaji magari na kuwaomba wadau kujitokeza kumuunga mkono kijana huyo ambaye ameonesha uthubutu na mafanikio yanaonekana.

Naye Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge amesema Edwin Charles amekuwa kijana wa mfano na amefanikiwa kujiajiri na kutoa ajira kwa vijana kupitia Kampuni yake ya uagizaji magari huku akiwaomba wadau kutumia fursa ya kampuni hiyo kutimiza ndoto zao kwa kuagiza magari kwa gharama nafuu.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company, Edwin Charles Dellah (katikati) akimkaribisha Paroko wa Parokia ya Ngokolo Jimbo Katoliki Shinyanga, Padre Adolf Makandago (kulia) katika ofisi Mpya za Kampuni ya Dellah Car Traders zilizopo katika Ghorofa ya Pili katika Jengo la NSSF Mjini Shinyanga. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company, Edwin Charles Dellah (kulia) akielezea huduma zinazotolewa na Kampuni ya Dellah Car Traders.
Paroko wa Parokia ya Ngokolo Jimbo Katoliki Shinyanga, Padre Adolf Makandago (katikati) na wageni waalikwa wakipiga picha ya kumbukumbu katika ofisi Mpya za Kampuni ya Dellah Car Traders zilizopo katika Ghorofa ya Pili katika Jengo la NSSF Mjini Shinyanga.
Paroko wa Parokia ya Ngokolo Jimbo Katoliki Shinyanga, Padre Adolf Makandago (kulia) na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge wakikata utepe kufungua rasmi ofisi Mpya za Kampuni ya Dellah Car Traders zilizopo katika Ghorofa ya Pili katika Jengo la NSSF Mjini Shinyanga.
Paroko wa Parokia ya Ngokolo Jimbo Katoliki Shinyanga, Padre Adolf Makandago (kulia) akiweka wakfu ofisi Mpya za Kampuni ya Dellah Car Traders zilizopo katika Ghorofa ya Pili katika Jengo la NSSF Mjini Shinyanga.
Paroko wa Parokia ya Ngokolo Jimbo Katoliki Shinyanga, Padre Adolf Makandago (kulia) akiomba baada ya kufungua rasmi ofisi Mpya za Kampuni ya Dellah Car Traders zilizopo Ghorofa ya Pili katika Jengo la NSSF Mjini Shinyanga.
Paroko wa Parokia ya Ngokolo Jimbo Katoliki Shinyanga, Padre Adolf Makandago akizungumza baada ya kufungua rasmi ofisi Mpya za Kampuni ya Dellah Car Traders zilizopo Ghorofa ya Pili katika Jengo la NSSF Mjini Shinyanga.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge akizungumza baada ya Paroko wa Parokia ya Ngokolo Jimbo Katoliki Shinyanga, Padre Adolf Makandago kufungua rasmi ofisi Mpya za Kampuni ya Dellah Car Traders zilizopo Ghorofa ya Pili Jengo la NSSF Mjini Shinyanga. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company, Edwin Charles Dellah akizungumza wakati wa sherehe za ufunguzi wa ofisi Mpya, Miaka mitatu ya Kampuni ya Dellah Car Traders na kumbukumbu ya kuzaliwa kwake Februari 28.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company wakijitambulisha ukumbini.
Muonekano wa Keki maalumu kwa ajili ya Sherehe ya Miaka Mitatu tangu kuanzishwa kwa Kampuni ya Dellah Car Traders Company pamoja na Kumbukumbu ya Kuzaliwa ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company, Edwin Charles Dellah
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company, Edwin Charles Dellah (katikati) akipiga makofi baada ya kuwasha mshumaa
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company, Edwin Charles Dellah akikata Keki maalumu kwa ajili ya Sherehe ya Miaka Mitatu tangu kuanzishwa kwa Kampuni ya Dellah Car Traders Company pamoja na Kumbukumbu ya Kuzaliwa ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company, Edwin Charles Dellah
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company, Edwin Charles Dellah akimlisha keki mmoja wa watoto 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company, Edwin Charles Dellah akilishwa keki na mtoto
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company, Edwin Charles Dellah akicheza muziki na watoto
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company, Edwin Charles Dellah akigawa juisi na biskuti kwa watoto
Wadau mbalimbali wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company wakiwa ukumbini
Burudani kutoka kundi la vijana maarufu 'Kambi ya Nyani' ikiendelea ukumbini.
Watoto wakiwa ukumbini
Wadau wakimwagia maji Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company, Edwin Charles Dellah kusherehekea siku yake ya kuzaliwa
Wadau wakimwagia maji Mkurugenzi wa Kampuni ya Dellah Car Traders Company, Edwin Charles Dellah kusherehekea siku yake ya kuzaliwa
Wadau wakiwa ukumbini
Wadau wakiwa ukumbini
Wadau wakiwa ukumbini
Wadau wakiwa ukumbini
Wadau wakiwa ukumbini

Wadau wakiwa ukumbini.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Post a Comment

0 Comments