Ticker

6/recent/ticker-posts

DKT. JAFO ATOA SIKU 14 KWA KINONDONI KUREKIBISHA MFUMO WA MAJI TAKA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimsikiliza Bw. Rajab Juma Mkazi wa Ufipa akielezea changamoto wanayoipata katika makazi yao kutokana na mfumo wa majitaka usio rafiki kwa mazingira. Dkt. Jafo ametoa muda wa siku 14 kwa Uongozi wa Wilaya ya Kinondoni kutatua tatizo hilo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Godwin Gondwe.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Wilaya ya Kinondoni kutatua kwa haraka tatizo la mfumo wa maji taka unaopita katika makazi ya watu ambao miundombinu yake imechakaa na kusababisha kero kwa wakazi wa Mtaa wa Ufipa. Kushoto mwenye miwani ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Godwin Gondwe.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Godwin Gondwe akissitiza jambo mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo mara baada ya Waziri huyo kufanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Ufipa kinondoni jijini Dar es salaam ambapo kuna kero ya utiririshaji maji taka katika makazi ya watu.

Picha ikionyesha miundombinu ilivyoharibiwa na mfumo wa maji taka ambao umepitta katika makazi ya watu wa Mtaa wa Ufipa ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameagiza eneo hilo kupatiwa ufumbuzi mapema.

Picha ikionyesha mfumo wa maji taka unaopita katika makazi ya watu pia miundombinu yake imechakaa na kusababisha kero kwa wakazi wa Mtaa wa Ufipa ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameagiza eneo hilo la Ufipa kupatiwa ufumbuzi mapema.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

******************

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametoa muda wa siku kumi na nne kwa Uongozi kwa Wilaya ya Kinondoni pamoja na DAWASA kuhakikisha wanatatua tatizo la mfumo wa majitaka katika Mtaa wa Ufipa Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Waziri Jafo ametoa agizo hilo leo 25/02/2022 mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Mtaa wa Ufipa na kujionea uharibifu mkubwa wa mazingira utokanao na mfumo wa maji taka ambao miundombinu yake imeharibika na kutiririsha maji taka katika makazi ya watu.

Akiwa katika eneo hilo Dkt. Jafo amesikitishwa na maelezo ya wataalamu wa DUWASA, TARURA na Manispaa ya Kinondoni kutokuwa na habari ya changamoto inayowakabili wakazi wa eneo la Ufipa.

“Wataalamu msikae Ofisini tu, tokeni mje msikilize na kutatua kero za wananchi, haiwezekani mimi Waziri wa Mazingira nitoke Dodoma kuja kukagua na kuleta ufumbuzi wa tatizo hili wakati ninyi mpo hapa kila siku” Jafo alisisitiza.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Godwin Gondwe amesema atahakikisha tatizo hilo linapatiwa ufufumbuzi ndani ya siku 14 kama Waziri Dkt. Selemani Jafo alivyoelekeza.

“Mhe. Waziri nikuhakikishie, sisi Wilaya ya Kinondoni kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi, siku ya Jumatatu yaani 28/02/2022 tutawasilisha kwako mpango kazi wa utekelezaji katika kutatua suala hili” Gondwe alifafanua.

Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa eneo hilo Rajab Juma amesema changamoto hiyo ya majitaka katika makazi yao ni ya muda mrefu na imekuwa ni kero hususan kipindi cha mvua ambapo majitaka hufurika na kuhatarisha usalama wa maisha yao pamoja na kukabiliwa na mlipuko wa magonjwa.

Post a Comment

0 Comments