Kampuni ya simu za mkononi ya itel imeachia smartphone mpya inayotoka kwenye kizazi cha “A” Series ambayo ni A58.
Taarifa rasmi iliyotoka ndani ya kampuni hiyo ni kwamba simu hiyo tayari imeingia sokoni na inapatikana nchini kote.
Msimamizi wa duka Mary Michael (kushoto) akimwelezea mteja kuhusu itel A58
Kuna mambo mapya na ya ziada ndani ya A58 ambayo ni pamoja na kuboreshwa zaidi kutoka toleo lililotangulia. Uwezo wa A58 ni wa kipekee zaidi kuanzia kwenye betri ambayo inamwezesha mtumiaji kutumia kupiga mziki mfululizo kwa muda wa siku tano pasipo kuzima. Hii ni sifa ya kipekee.
Vipengele vingine muhimu ndani ya itel A58 ni pamoja na kuwa na mfumo endeshi wa Android 11 Go, uwepo wa kamera mbili za nyuma, na skana ya alama za vidole yaani fingerprint sensor.
Ikilinganishwa na toleo la awali lililotangulia, itel A58 imekuja na maboresho ya kisasa kabisa yanayoleta fahari kwa mtumiaji. Maboresho hayo ni pamoja na kuongezeka kwa skrini ambayo ni 6.5” pia imekuja na skrini yenye ‘waterdrop’ inayokuza mwonekano mzuri zaidi wa simu hii.Cleophas Mapunda (kulia) Meneja mauzo wa itel kanda ya Dar es Salaam akiielezea itel A58 pamoja na Promosheni inayoendelea.
Imethibitishwa na meneja mauzo kanda ya Dar es Salaam Cleophas Mapunda kuwa simu hiyo inafanyiwa promosheni nchini kote ambapo wateja wanaonunua A58 watapatiwa zawadi ziliazoandaliwa katika vituo vya promotion na pia ‘road show’ inayoendelea nchi nzima.
“Katika msimu huu wa Valentine itel mobile inakuletea simu bomba ya A58 huku tukiwa na promosheni kabambe sana na road shows ambayo mteja utaweza kujipatia zawadi Kem Kem kama birika, mto, kofia n.k” Amesema Mapunda.
Kwa upande mwingine naye meneja wa mfumo wa manunuzi mtandani wa itel unaojulikana kama egatee, Bwana Godwin Uledi, ameeleza kuwa kwa wafanyabiashara watakatoa oda ya itel A58 mbili kupitia mfumo huo wa egatee wataweza kupatiwa punguzo la bei pamoja na zawadi ya speaker ya redio bure.
Godwin Uledi, Meneja wa mtandao wa egatee
Akifafanua kuhusu mfumo huo, Godwin amesema, “Egatee ni App mpya na ya kijanja kabisa ambayo inalenga kuwasaidia na kuwarahisishia wateja wa rejareja kuweza kupata bidhaa za itel kwa bei nafuu na kujishindia zawadi kemkem kupitia sera kwa kila mwezi” Amesema Godwin.
Kupata taarifa zaidi ya itel A58 tafadhali tembelea kurasa zetu za mtandaoni itel Tanzania au bofya https://www.instagram.com/iteltanzania/
0 Comments