...............................................
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaounda Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo mara baada ya kufanya ziara katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road wamemtembelea Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mikumi Bw. Joseph Haule Maarufu kwa jina la Prof J aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili @muhimbili_taifa Jijini Dar es Salaam.
Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuelekeza Serikali igharamie matibabu ya Prof. J, nawapongeza Madaktari na Uongozi wa Hospitali kwa kuhakikisha hali ya afya ya Prof. J imeendelea kuimarika, tuendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona” amesema Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya.
“Hali ya Prof J imeendelea kuimarika na hivi sasa anaendelea vizuri na ametutambua wote kwa majina, tupuuzie maneno yanayozushwa mitandaoni” amesema Mhe. Shabani Hamisi Taletale Mbunge wa Jimbo la Kusini Mashariki (Morogoro)
0 Comments