Ticker

6/recent/ticker-posts

KATIBU MKUU DKT. CHAULA AZIFUNDA ASASI ZA KIRAIA-NGOs


KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Dkt. Zainab Chaula kushoto akizungumza wakati wa kikao hicho wa kwanza kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira.
Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira
Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira akisistiza jambo wakati wa kikao hicho

Mkutano ukiendelea



****************

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Dkt. Zainab Chaula amekutana na Asasi za Kiraia AZAKI kutoka Mikoa ya Dodoma, Singida na Iringa lengo likiwa kujadili juu ya Ustawi wa taasisi hizo nchini



Mkutano huo ulifanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma huu ni utekelezaji wa ombi la Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira kuhusu Wizara hiyo kukutana na NGOs za Mikoani na ombi hili aliwasilisha alipokutana na Katibu Mkuu huyo Januari 24 mwaka huu.



Akizungumza wakati wa kikao hicho Katibu Mkuu Chaula amesema kikao hicho na mambo mengine kimelenga kupokea changamoto, kutoa elimu ya namna ya kuendesha AZAKI kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu ikiwemo kukabiliana na namna ya kuimarisha sekta hiyo.



Ameongeza kuwa kikao hicho kimetoa fursa kwa AZAKI kutoka mikoani kutoa maoni yao na kupata uwakilishi katika vikao na wizara kutokana na kwamba Asasi hizo zimekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Tanzania.



Ambapo zimekuwa zikitoa elimu kwa wananchi kuhusu mipango mbalimbali ya Serikali ikiwemo mabadiliko ya Tabia ya nchi, masuala ya kiafya na kidemokrasia.



Akizungumza wakati wa Kikao hicho ,Mbunge Neema Lugangira amesema lengo ni kutoa fursa kwa NGOs za mikoani kutoa maoni yao na kupata uwakilishi katika vikao na Wizara



Alisema pia lengo lengine ni kupokea changamoto, kutoa elimu ya namna ya kuendesha NGOs kwa kufuata sheria na kanuni na taratibu na kukubaliana namna ya kuimarisha Sekta ya Azaki.

Post a Comment

0 Comments