Ticker

6/recent/ticker-posts

KMC YAIFUNGA POLISI TANZANIA MABAO MATATU BILA JANA, KUANZA MAZOEZI KESHO KUWAKABILI COAST UNIONI JUMAPILI*********************

Kikosi cha KMC FC jana kimeanza vema mzunguko wa Pili wa Ligi kuu ya NBC soka Tanzania bara baada ya kuibuka na ushindi wa magoli matatu kwa sifuri dhidi ya Polisi Tanzania mchezo uliopigwa katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi Jijini Dar es Salaam.

Magoli hayo bora ya ushindi kwa KMC FC yamefungwa na Iddi Kipagwile, Emmanuel Mvuyekule pamoja na Sadala Lipangile na hivyo kufikisha jumla ya alama 22 na kupanda kwenye nafasi ya sita mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC kutoka nafasi ya 11 iliyokuwa awali kabla ya mchezo huo wa jana.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa saa moja jioni, ulikuwa na ushindani mkubwa kutokana na historia ya Timu hizo mbili pindi zinapokutana kuwa na ushindani mkubwa tangu zilivyopanda kushiriki michuano ya Ligi Kuu soka Tanzania huku Polisi Tanzania ikipata matokeo zaidi dhidi ya KMC FC.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu Thierry Hitimana imekuwa na muendelezo mzuri wa kupatamatokeo ikiwa ni mkakati wa Viongozi, Benchi la ufundi pamoja na wachezaji kuhakikisha kwamba inafanya vizuri kwenye kila mchezo na hivyo kuendelea kutafuta nafasi tatu za juu kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC.

Aidha matokeo ya mchezo huo wa jana yametokana na ubora wa wachezaji Benchi la ufundi ikiwa ni muendelezo mzuri wa KMC kupata matokeo ya kushida mechi mfululizo ambapo kwenye mchezo wa kufunga mzunguko wa kwamba ili inuka na ushindi wa magoli ma wili kwa sifuri dhidi ya Dodoma Jiji na kwamba jitihada hizo zitaendelea ili kufikia malengo ya klabu iliyojiwekea.

“Tumeanza vizuri mzunguko wa pili, hizi nijitihada kubwa ambazo wachezaji wetu wanafanya wakiwa kwenye mazoezi lakini pia kufuata maelekezo ya mwalimu anayoyatoa, tunahitaji kuendeleza ubora huu kwa kila mechi ambayo tutacheza, hivyo kikubwa tunazidi kumuomba Mungu awape Afya njema wachezaji wetu kila siku.

Kwenye mzunguko wa kwanza hatukuanza vizuri, na Tulipoteza dhidi ya Polisi Tanzania kule Karatu, kwa hiyo kwenyemzunguko huu tuliweka nia kabisa kwamba hatuhitaji kupoteza tena ,wachezaji walijituma zaidi na mwisho wa siku tukapata matokeo hilo ni jambo jema tunawapongeza zaidi wachezaji kwa kazi kubwa wanayoifanya.

KMC FC kesho itaanza tena maandalizi ya mchezo mwingine dhidi ya Coast Union utakaopigwa siku ya Jumapili ya Machi saba hapa Jijini Dar es Salaam na kwamba uongozi umetoa mapumziko leo Jumapili na kesho jumatatu asubuhi program ya mazoezi itaanza kama ambavyo kocha Mkuu Hitimana ameandaa.

Imetolewa leo Februali 27

Na Christina Mwagala

Afisa Habari na Mawasiliano KMC FC

Post a Comment

0 Comments