***************************
Tuanze na swali rahisi tu Je, mirabaha ni nini kwa wasanii na wabunifu wengine?
Jibu: Mirabaha ni kama fidia anayolipwa mbunifu (awe msanii wa muziki, filamu, mgunduzi wa programu ya kompyuta, mtunzi wa kitabu na/au kazi nyingine yoyote ya ubunifu inapotumiwa na mtu mwingine kibiashara “economic rights” au wakati fulani ni fidia ya msanii na mbunifu pale kazi yake inapotumika isivyopaswa “moral rights.”). Nitafafanua.
Sheria ya Tanzania ya Mwaka 1999 (The Copyrights and Neighbouring Rights Act, 1999), inatoa haki kuu mbili: kwa mmiliki wa kazi yenyewe (primary rights) lakini inawapa pia haki flani walioshiriki katika ubunifu husika iwapo, kimkataba, hawakumalizana kimalipo na mhusika na hivyo kupewa “hisa” katika ubunifu huo. Hii huitwa “neighbouring rights.”
Neighbouring rights hapa zinaweza kuwa kama vile haki ya maproducer katika wimbo, mtunzi wa wimbo
na katika nchi nyingine inaangaliwa hata waliodansi (wacheza show) na mavideo vixen walionogesha video ya wimbo husika.
Swali: Je, mrabaha ni sawa na mauzo ya kazi za msanii???
HAPANA: Tena HAPANA! Na hili wasanii na Watanzania waelewe. Taasisi za Copyrights hazihusiki na mauzo ya kawaida ya kazi za msanii au mbunifu yeyote.
Kwa mfano: Diamond anapotoa wimbo na kuuweka Boomplay kuuza kule analipwa na kumalizana na wahusika sawa na enzi zile msanii wa filamu anapeleka filamu kwa kampuni ya STEPS inauzwa kisha yanagawanywa mapato.
Hakimiliki inakwenda mbali baada ya mauzo ya kawaida ya kazi.
Mfano mwingine: mtu kanunua album ya Alikiba-hapo Kiba ananufaika na mauzo moja kwa moja. Lakini aliyenunua album ya Alikiba anapaswa aitumie kwa ajili yake na hata jamaa zake tu. Haya yanaitwa matumizi kusudiwa.
Sasa ukitumia albumj hiyo kuziweka nyimbo kwenye flash au ukazalisha album zaidi kuuza hapo dhana ya hakimiliki na mirabaha inakuja.
Msanii wa riwaya anapoandika kisha mwingine akanunua kitabu husika mpaka hapo mapato ya msanii yako kwenye mauzo tu.
Lakini mwigizaji anapochukua riwaya hiyo na kuitengenezea script na kuitumia kuigiza filamu yake, hakimiliki ya yule mwenye kitabu inapaswa kulipwa na dhana ya mrabaha huibuka hapo.
Kwa kifupi wasanii waendelee kuuza kazi zao, mirabaha sio mbadala wa mauzo na nasiaitiza mrabaha si mauzo bali ni pato la ziada IWAPO, nasisitiza tena, IWAPO, mifumo ya taasisi za Hakimiliki itabaini kutumika kwa kazi yako kibiashara na kukukusanyia mapato yako. Maana yake pia hapa unaweza kuwa msanii nguli lakini kazi yako ikawa inauzwa sana moja kwa
moja lakini ukawa hauna mrabaha sababu haijatumika kiuchumi.
Hii inaeleza ni kwa nini sio kila mtu aliyesajili kazi yake tu Cosota anapaswa kulipwa mirabaha, HAIWEZEKANI, na hii inaeleza ni kwa nini pia hata waliosajili kazi zao na zikatumika kibiashara bado watatofautiana malipo kutokana na wingi (freguency) ya kutumika kazi zao iwapo, kwa mfano, kipimo ni matumizi hayo kwenye radio!
Shauri la Fox News Vs TvEyes la nchini Marekani linaweza kutosha kutusaidia kuona dhana ya “economoc usage.” Katika shauri hilo la mwaka 2018 kampuni ya Fox ilidai fidia ya kimrabaha kufuatia kampuni hiyo kukusanya vipindi mbalimbali vya TV na kuviwela katika mfumo wa kuviuza tena bila hata kuomba leseni kwa Fox News.
Mahakama ya Rufaa iliamua kuwa Fox Newe kwanza walipaswa kuwa wameridhia matumizi hayo ya
maudhui yao original
kuwekwa kwenye platform nyingine na kuuzwa (moral right) na pili walikuwa na haki ya
kulipwa mrahaba (economic usage).
Tufahamu pia kwamba kwa
mujibu wa kifungu cha 14 cha Sheria ya Tanzana ya Mwaka 1999 kinasisitiza haki hizi hudumu katika muda wote mhusika akiwa hai na walau miaka 50 tangu afariki au miaka 50 tangu afariki msanii/mmiliki wa mwisho kama ilikuwa ni “collabo.” Hivyo wasanii watilie
mkazo!
Wasanii na wabunifu pia wasome sana kifungu cha 15 kinachoonesha mikataba mbalimbali katika kumiliki kwa pamoja au la kazi hizi.
Mfano itakuwa maajabu kwa kifungu hicho kama msanii wa dansi kwa mfano wa Band A, kalipwa na bosi wake akatunga wimbo wakaurekodi ukachezwa sana, lakini kwa kuwa alishalipwa kwa kazi yake, wimbo ule ni wa Band na sio wa msanii aliyeimba hivyo ikitokea matumizi ya kiuchumi malipo yatakwenda kwa Band husika (hapa wasanii wawe makini mikataba wanayosaini usiposema vinginevyo haki inabaki kwa Band).
KWANINI SAMIA SANAMU LINAMHUSU
Sheria hii haikutekelezwa ipasavyo tangu ianze ingawa sasa tunaona mwelekeo mzuri.
Moja ya kosa nadhani ni mifumo ya
makusanyo iliyokuwepo kutozibana redio zikaonekana eti zinapiga tu muziki kupromote wasanii, hii imesababisha wengi kukosa kipato.
Sasa chini ya Rais Samia redio na TV zimeanza kulipa kwa kazi wanazocheza na ndio maana katika malipo ya juzi nimesikia wataalamu wa Cosota wanasema wametumia “logsheets” kwa sampuli ya kitaifa, kikanda, redio za dini na za mahadhi ya muziki wa zamani.
Serikali kweli imesimama kidete na kushinda hii vita ambayo huko nyuma wamiliki wa radio waliishinda na wakabaki salama!
Hii inaeleza ni kwa nini juzi TZS 312m zimegaiwa kwa wasanii na wabunifu mbalimbali huenda zikiwa ni hela nyingi zaidi kuwahi kutolewa kama mirabaha kwa wabunifu nchini tangu Uhuru.Kongole Mama!
Tuendelee kumtia moyo Mama
Samia na watendaji wake kwa mara ya kwanza nikiwa mfuatiliaji wa
masuala ya Hakimiliki haki imetendeka.
Huko nyuma ilikuwa hela inayopatikana inagawanywa kwa watu wote waliosajili tu kazi zao Cosota-hii haikuwa haki ilisababisha wasanii ambao kazi zao zimetumika sana kuishia kupata laki 2 au tatu na wengine kushuka mpaka elfu 10!
Leo sheria na dhana ya “economic usage” imetumika ndio maana unaona Alikiba kapata zake 7.5m wale kwaya ya Mt. Cecilia wameondoka na 8m na wasanji wengine wote wakubwa Diamond, Zuchu, Nandy, Harmonize, Marioo, maproducer kama P Funky, wasanii wa zamani kama Ali Choki, Abdul Misambano na wengine wote wana hela nzuri tu katika orodha iliyotolewa japo kwa viwango tofautitofauti!
Tulikuwa tunadanganyana kwa kugawana wote hii ni hatari maana yake ingekuwa sasa kila mtu anawahi studio anarekodi wimbo wa hovyo hata 10 anawahi Cosota anazisajili anasubiri mgao hata kama kazi hake hizo hazijatumika popote kibiashara!!! Hii imewapunja sana wabunifu stahiki zao kwa miaka mingi.
Nihitimishe: wasanii na wabunifu wengine wabuni kazi bora na wakazisajili. Lakini wasiishie hapo ili kupata hela kwa mifumo ya sasa wazisambaze na kuzipromoti kazi zao kwenye radio na tv ili zichezwe sana, huko ndio kuna hela! Na waliokosa safari hii wajipange kwa safari ijayo.
Ndio maana nasema kwa Kanuni hii mpya iliyotumika katika
mirabaha, Mama Samia Ajengewe Sanamu Kibaha
0 Comments