Ticker

6/recent/ticker-posts

WILAYA YA IKUNGI YAJIVUNIA MAFANIKIO KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 45 YA CCM

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Mika Likapakapa ,akihutubia wananchi na Wana CCM katika sherehe za kuadhimisha miaka 45 tang kianzishwe chama hicho Februari 5, 1977 zilizofanyika kiwilaya Kata ya Iglanson.

Mkuu wa wila hiyo Jerry Muro akizungumza kwenye sherehe hiyo.

Katibu wa CCM wa wilaya hiyo Stamili Dendego akizungumza kwenye hafla hiyo
Katibu Mwenezi wa CCM wa wilaya hiyo, Pius Sanka akiongoza sherehe hizo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Mika Likapakapa akishiriki kupanda mche wa miti katika eneo la la kituo cha afya cha Kata ya Iglanson ikiwa ni moja ya shughuli za sherehe hiyo.
Katibu Mwenezi wa CCM wa wilaya hiyo, Pius Sanka akipanda mche wa mti.

Katibu wa CCM wa wilaya hiyo Stamili Dendego akishiriki kupanda mche wa mti.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa wa wilaya hiyo Shabani Dude akipanda mche wa mti.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi Jafari Dude akishiriki kupanda mche wa mti.
Katibu wa Umoja wa Jumuiya ya Wazazi wa wilaya hiyo Bwanga Akida Tayari akishiriki kupanda mche wa mti.
Mche wa Mti ukipandwa.
Wana CCM wakionesha miche ya miti wakati wa zoezi la kuipanda.

Muonekano wa kituo cha afya cha Kata ya Iglanson kinachoendelea na ujenzi.


Vijana wa UVCCM wakioneshana jengo la kituo cha afya la Kata ya Iglanson.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally Mwanga akishiriki kupanda mche wa mti.

sherehe zikiendelea.

Sherehe zikiendelea.




Vijana wakiwa kwenye sherehe hizo.


Mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Iglanson, Bwana Elifuraha akizungumza kwenye sherehe hizo.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Abubakar Muna akizungumza kwa niaba ya mbunge huyo kwenye sherehe hizo.

Burudani zikitolewa na wasanii wa kata hiyo Kushoto ni Katibu wa CCM wa wilaya hiyo Stamili Dendego.

Burudani zikiendelea.

Burudani zikiendelea.

Wanakina mama na watoto wao wakiwa kwenye sherehe hizo.

Baadhi ya madiwani na wananchi wakiwa kwenye hafla hiyo.

Furaha kwenye sherehe hiyo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Mika Likakapa akimkabidhi kadi ya chama hicho Malando John aliyehamia cha hicho.

Taswira ya mkutano huo.
Mwanachama mpya wa CCM Malando John (kulia aliyejifunga kanga ya akila kiapo.

Madiwani wa Viti Maalumu wa Wilaya ya Ikungi wakiwa kwenye sherehe hizo. Katikati ni Diwani Zainabu Hassan na kushto ni Diwani Margareth Gwau.






Diwani wa Kata ya Iglanson Yusuph Athumani akisebuba sambamba na msanii wa kikundi cha Sanaa cha Nyanda Moja moja.

Kada wa CCM wa Wilaya ya Ikungi kutoka Kata ya Iglanson Joseph Ngerera Mwinamila (kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro wakati wa sherehe hiyo walipo mtembelea nyumbani kwake. Katika ni Mwenyekiti wa CCM Mika Likapakapa.

****************************

Na Dotto Mwaibale, Singida

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa amesema wilayo hiyo Ikungi inajivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 45 tangu kuzaliwa kwa chama hicho Februari 5, 1977.

Akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya miaka 45 tangu kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika kiwilaya Kata ya Iglanson jana alisema baadhi ya mafanikio wanayojivunia ni miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanywa na serikali kwa gharama kubwa si kwa Ikungi tu bali kwa nchi nzima ambapo alimtaka kila kiongozi katika wilaya hiyo kuyatangaza mafanikio hayo ya Serikali ya kwanza hadi ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ili wananchi wayajue kwa kuiletea maendeleo wilaya hiyo kupitia miradi ya mbalimbali.

Alisema kila kiongozi ana wajibu wa kuisaidia Serikali kuyatangaza mafanikio hayo wananchi wayajue kwani bila ya kufanya hivyo wanaweza wakaibuka wajanza na kuanza kueleza ya na kupotosha ukweli wa kazi kubwa iliyofanywa na serikali.

Alitaja baadhi ya miradi waliyoipata ni ya ujenzi wa vituo vya afya na zahanati, maji, shule na miundombinu ya barabara.

Alisema katika wilaya hiyo wana vituo vya afya Kata za Irisya, Ntuntu, Iglanson ambavyo vipo hatua ya ujenzi wa Sh. 500 Milioni huku Kituo cha afya cha Sepuka na Ihanja vikiwa vimekamilika na hiyo yote ni kutokana na usimamizi mzuri ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM.

Likapakapa alitumia nafasi hiyo kuwataka wenyeviti wa vijiji kila mwaka kuitisha mikutano na kuwasomea mapato na matumizi ya fedha kama sheria inavyoelekeza na si vinginevyo.

Mkuu wa Wilaya hiyo Jerry Muro alisema moja ya jambo kubwa wanalojivunia sisi Serikali katika kipindi cha miaka 45 tulioyafanya na kumshukuru Mungu ni kusimamia usalama wa wananchi,mali zao na amani ya nchi yetu.

"Nataka kuwahakikishia kuwa kumlinda raia na mali zake watu waamke asubuhi waende mashambani, makazini, warudi nyumbani wapitie sehemu kupata kiburudisho na kurudi nyumbani salama sio jambo dogo kwani vijana wa usalama wanakuwa nje wakati wote kuwalinda.

Alisema mpaka tunafikia miaka 45 katika wilaya hiyo hakuna matukio yoyote makubwa ya kihalifu yaliyotokea ya uvamizi wa silaha, unyang'anyi na mauaji makubwa ya halaiki na wizi ni jambo la kujivunia sana na kuwa na Taifa lenye amani sio kazi ndogo kwani kuna mambo makubwa yanafanywa na vyombo vya usalama kuhakikisha nchi inakuwa salama na utulivu.

Muro alisema katika kipindi hiki cha miaka 45 wameshuhudi CCM ikikiisimamia Serikali na kuielekeza katika miradi yote mikubwa ya maendeleo na kuwa katika kipindi hiki cha miaka 45 mingine Serikali itahimalisha mtandao wake na kuhakikisha amani inaendelea kuwepo hapa nchini.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally Mwanga alisema katika kipindi hiki cha miaka 45 wanajivunia kuona Serikali ikitoa fedha nyingi za miradi mbalimbali katika wilaya hiyo na kueleza katika Shule Shikizi ya Isingisha walipata Sh.80 Milioni,Mwaru Sh.80 Milioni, Kizugi Sh.80 Milioni, Mnyange Sh.Milioni 40,Sekondari Sh.40 Milioni, Maji Iglanson Sh. 217 Milioni, Kituo cha Afya Kata ya Iglanson Sh.250 Milioni, Shule ya Msingi Iglanson Sh.53 Milioni, Maabara ya sekondari Sh.30 Milioni alisema fedha hizo karibu zaidi ya bilioni 1 zimetolewa na Serikali katika kata moja tu.

Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi Stamili Dendego akimkaribisha mgeni rasmi wa sherehe hiyo alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi wa kata hiyo kwa kufika kwa wingi na kueleza kuwa sherehe hizo katika wilaya hiyo zilianza Januari 24 na kuwa jumuiya ya vijana waliadhimisha sherehe hizo katika Kata ya Ntuntu, na Jumuiya ya Wazazi walihitimisha Kata ya Mkiwa huku UWT huku UWT wakihitimisha Kata ya Ikungi na kuwa leo Januari 2 kilele cha maadhimisho hayo kiwilaya yatafanyika katika Kata ya Mang'onyi.

Dendego alisema katika maadhimisho hayo kazi zilizofanyika ni kufanya usafi, kupanda miti kuzungunga Kituo cha Afya kinacho jengwa katika kata hiyo na kuingiza wanachama sambamba na kusajili watu kwa mfumo wa kielektoniki.

Post a Comment

0 Comments