**********************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Bw. Uledi Abbas Mussa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kwa kipindi cha miaka mitatu (3).
Bw. Mussa ni Katibu Mkuu Mstaafu na Mshauri Binafsi wa Masuala ya Kiuchumi wa Kimataifa (GFA Consulting Group), tawi la Tanzania.
Bw. Mussa anachukua nafasi ya Dkt. Suleiman Magesa Misango ambaye ataendelea na majukumu yake ya Ukurugenzi ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Uteuzi huu umeanza tarehe 23 Desemba, 2021.
0 Comments