Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZAZI SINGIDA WAOMBWA KUWARUHUSU WATOTO KUJIUNGA NA SKAUTI

Kijana wa Skauti akitoa maelezo ya shughuli zinazofanywa na chama hicho wakati wa maadhimisho ya siku ya Mwanzilishi wa Skauti Duniani Baden Powells yaliyofanyika Shule ya Msingi ya Kindai iliyopo Manispaa ya Singida mwishoni mwa wiki.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida akitoa mafunzo ya jinsi ya kujiokoa na majanga mbalimbali katika maadhimisho hayo. Kushoto mwenye Skafu ni Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick Ndahani.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida akitoa mafunzo ya jinsi ya kuzima moto.
Maadhimisho hayo yakiendelea. Wa pili kushoto mbele aliyevaa Skafu ni Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick Ndahani akiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mafunzo ya uzimaji moto yakifanyika kwenye maadhimisho hayo.
Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick Ndahani akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Vijana wakiserebuka kwenye maadhimisho hayo.
Mafunzo ya kuzima moto yakifanyika.


Picha ya pamoja.


**********************

Na Dotto Mwaibale , Singida


AFISA Vijana Mkoa wa Singida Frederick Ndahani amewaomba wazazi katika mkoa huo kuwaruhusu watoto wao ambao ni wanafunzi kujiunga na Chama cha Skauti Tanzania.

Ndahani alitoa ombi hilo katika kikao cha wazazi wa wanafunzi wa skauti katika Manispaa ya Singida waliokuja kujionea shughuli mbambali za vijana wa skauti katika siku ya mwanzilishi wa Skauti Duniani Baden Powells kilichofanyika katika Shule ya Msingi ya Kindai iliyopo Manispaa ya Singida.

Ndahani alisema skauti ni chama kinachowajenga wanafunzi kuwa wakakamavu,wazalendo,waminifu kwa jamii na Taifa, na kuwa na uwezo wa kupambana na majanga ya moto na mbinu za kuzuia Rushwa nchini.

"Wazazi tunaowajibu mkubwa kuhakikisha vijana wetu wanajengwa katika misingi hiyo,wapo wazazi amabo bado hawaoni umuhimu wa watoto wao kujiunga na chama hiki"alisema Ndahani.

Ndahani alisema kuwa mlezi wa chama cha skauti ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wake ni Waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia hivyo chama hicho kinasimamiwa kwa makini na kwa misingi yote.

Katika siku hiyo wanachama wa chama cha skauti wamepanda miti 350 katika Hospitali ya Rufaa na wazazi na wanachama wa skauti wamepata mafunzo ya namana ya kujikinga na kuzuia majanga ya moto yaliyotolewa na Jeshi la Zima Moto na mafunzo ya kupambana na Kuzuia Rushwa yaliyotolewa na TAKUKURU Wilaya ya Singida.

Aidha wazazi wamejionea mambo mbalimbali yaliotengenezwa na vijana katika kambi ya mfano ikiwemo jokofu la asili la kuhifadhia maji,meza na kiti cha asili pamoja na jiko ambalo unaweza kupikia katika ya mto wenye maji.

Kwa upande wao wazazi wameushukuru uongozi wa skauti, Jeshi la Zmamoto na Uokoaji pamoja na TAKUKURU kwa kuendesha kikao na mafunzo hayo na wameahidi kuwa mabalozi wazuri kwa jamii juu ya umuhimu wa wanafunzi na watoto kujiunga na chama hicho kwa sababu vitu na mambo wanayojifunza vijana si kwa faida yao tuu bali ni kwa familia, jamii na Taifa kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments